HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2019

ALUMNI WA MZUMBE WAKUTANISHWA KIDIGITALI, MKUTANO MKUU KUUNGURUMA NOVEMBA 21

Na John Marwa, Dar es Salaam

CHUO Kikuu Mzumbe kinawaalika Alumni wake wote nchi nzima kwa maana ya wahitimu katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 19, wa Baraza la Wahitimu na Baraza la Masajili ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 21 Mwaka huu, Kampasi Kuu Mzumbe.
Mkutano huo utawakutanishi wale wote ambao walisoma Mzumbe na iliyokuwa IDM zamani, wenye lengo la kujadili mambo mbali mbali ya chuo hicho pamoja na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika mkutano wa Alumni wa Dar es Salaam Aloyce Gervas, ‘Alumni’ ambaye sasa ni Mhazidhiri  msaidizi na mratibu wa mkutano huo jijini Dar es Salaam, alisema yeyote yule aliyesoma Chuo Kikuu Mzumbe au iliyokuwa IDM zamani basi anaalikwa kuhudhuria mkutano huo.
“Kwa yeyote yule ambaye amewahi kusoma Mzumbe ama iliyokuwa IDM zamani, tunamwalika kwa upendo mkubwa aweze kuja kushiriki pamoja nasi katika mkutano huo, ili tuweze kujadili mambo  mbali mbali ambayo tunaweza tukasaidiana kuyafanya kwa mustakabali wa kukijenga chuo chetu.
“Lakini pia kulijenga Taifa letu na kuungana pamoja na Rais wetu Mpendwa Dk. John Magufuli, katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu na gurudumu la maendeleo katika chuo chetu.”alisema Gervas na kubainisha kuwa.
“Kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo tupende kuwaalika rasmi Alumni wetu wote popote pale walipo waweze kushiriki Mkutano huo.”alisema.
Katika hatua nyingine Gervas alieleza kuwa, Chuo Kikuu Mzumbe kimeona kiweze kuwafikia wahitimu wake wote kwa maana ya Alumni nchi nzima kwa kuunda makundi maalumu kila Mkoa na makundi hayo kuweza kuwaunganisha wale wote walio soma Mzumbe ama iliyokuwa IDM zamani.
“Kwa makundi hayo kwa kutumia Whatsapp tumekuwa tukiwaunganisha wote popote pale walipo katika maeneo mbali mbali ambayo wanafanyia kazi, kwa kufanya hivyo tukaona tuwe na mikutano ya makundi hayo kwa wanachama wote waliojiunga leo (jana, Novemba 10, 2019.
“Katika mikutano yetu hii ambayo tumeifanya maeneo mbali mbali nchi nzima kwa maana hapa Dar es Salaam Kampusi ya Mzumbe, lakini pia Mwanza, Mbeya, Dodoma Arusha na maeneo mengine nchini.
“Malengo yetu makubwa ni kuunganika nao kutaka kufahamu waliko na wao wafahamu Chuo tunafanya nini katika maendeleo ya nchi yetu na katika kukiendeleza chuo chenyewe, na wao kama Alumni wetu tufahamu yale ambayo wanayafanya, walipofika na zile stori mbalimbali za mafanikio yao basi waweze kutushirikisha ama tushirikishane kwa pamoja ili tuweze kuona ni wapi ambapo tunaweza tukasaidia na wao waweze kurudisha mchango wao kwa chuo kwa yale ambayo chuo kiliwafanyia mpaka kuweza kufika hapo walipo fika.” Aliongeza kuwa
“Tumekuwa na viongozi mbali mbali wa hayo makundi ambapo na wao pia wanahamasika ama kuhamasisha watu wengine wazidi kujiunga na makundi haya, kutakuwa na mikutano endelevu mbali mbali maeneo mbali mbali ambapo tutakuwa tukikutana kwa ajili ya majadiliano.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Mzumbe Alumni) waishio Dar es Salaam wakianza kwa sala kikao cha kwanza cha wahitimu kilichoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na kufanyika katika Kampasi ya Dar Es Salaam Novemba 10, 2019. .

Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe, Prof Honest Ngowi, akisisitiza jambo katika kikao cha kwanza cha wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe waishio Dar es salaam , Kilichofanyika Novemba 10, 2019, Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Muda wa Alumni wa Dar es Salaam Bw. Kapufi Yusufu Ally, akiongoza Mkutano wa Alumni wa Cluster ya Dar Es Salaam , Aliyeketi (katikati) ni Katibu Bw. Amani Mwanga ,na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kampasi ya Dar Es Salaam Prof. Prosper Honest Ngowi.

Bw. Obed Kasambala Alumni Chuo Kikuu Mzumbe akichangia mjadala wa njia za kukutanisha wahitimu katika chuo Kikuu Mzumbe wanaoishi Dar es Salaam.

Washiriki wakifuatilia mjadala.

 
Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam Prof. Prosper Honest Ngowi katika picha ya pamoja na Alumni wa Cluster ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages