MKE
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa wito kwa wazazi na walezi
watoto wenye mahitaji maalumu kutowaficha na kuwatelekeza na badala
yake wawape nafasi ya kupata elimu kwa sababu ni haki yao ya msingi.
Mama
Majaliwa ambaye pia ni Mlezi wa Umoja wa Wake wa Viongozi (New
Mellenium Women Group), ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 10,
2019), wakati alipokabidhi majengo ya madarasa manne na matundu ya vyoo
kumi kwa Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu cha Buhangija mkoani Shinyanga
yaliyojengwa na umoja huo.
Mama
Majaliwa amesema si vyema kuwatenga au kuwakatia tamaa watoto wenye
ulemavu kwani wao pia ni watoto sawa na watoto wengine, hivyo
wanastahili kupewa haki zote bila kubaguliwa.
Amesema
hatua waliyochukuwa akinamama wa umoja huo inaunga mkono jitihada za
serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
za kuwapatia watoto wa kitanzanai elimu bure na katika mzingira mazuri.
Mgeni
rasmi katika makabidhiano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na
Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako ameupongeza umoja huo kwa
shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwajali watoto wenye mahitaji
maalumu.
Profesa
Ndalichako amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Serikali
imetenga jumla ya sh 3,809,758,460.00 kwa ajili ya kununua na
kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vifaa
visaidizi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (wakiwemo
Albino), katika shule na vitengo vya elimu maalum.
Waziri
huyo ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo za Serikali, bado
wanafurahi wanapopata michango kama huo uliotolewa leo. "Wito wangu
kwenu tusichoke kuwasaidia hawa watoto wetu. Napenda kuwakumbusha
na kusisitiza kwamba Watu wenye Ulemavu wanahitaji msaada mkubwa
kutoka kwenu."
"Tuwasaidie
na tushirikiane kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwa ni pamoja
na elimu, huduma za afya na mazingira mazuri ya kuwawezesha
kuishi bila ya matatizo. Serikali kwa upande wake itaendelea
kujitahidi kwa uwezo kutoa fursa zinazojali mahitaji yao."
Amesema
madarasa pamoja na vyoo alivyokabidhiwa leo kwa niaba ya uongozi
wa kituo cha Buhangija na Kikundi cha New Millenium ni tunu kwao
na wananchi wa Shinyanga na ni sadaka kwa watoto wa Buhangija,
hivyo, ameutaka uongozi wa Mkoa na Uongozi wa Kituo kwa pamoja
washirikiane kuyatunza vizuri ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.
Akitoa
taarifa ya ujenzi huo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga, Albert Msovela amesema fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi
wa madarasa manne ni sh. 65m,884,523/= ambapo kila chumba cha darasa
kimejengwa kwa wastani wa sh. 16,471,130.
Amesema
ujenzi wa vyumba kumi vya vyoo unaendelea na ukikamilika utagharimu
sh.26, 271,922.44 na kwamba vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa vikiwa na
maji ndani pamoja na masinki ya kunawia ili kukidhi mahitaji ya watoto
wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment