Dk. Amos Nungu |
Na Suleiman Msuya
WANASAYANSI
kutoka nchi 15 za Kusini mwa Jangwa la Sahara, taasisi na nchi rafiki duniani
wameshauri Serikali mbalimbali kuongeza uwekezaji katika shughuli za utafiti na
ubunifu ili kutatua changamoto kwenye jamii.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolijia (COSTECH), Dk. Amos
Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano huo wa Baraza la Sayansi Kanda ya Afrika
unamalizika leo jijini Dar es Salaam.
Alisema
mkutano huo mkuu wa mwaka ambao umeshirikisha wajumbe zaidi ya 250 umekuwa wa
mafanikio makubwa kwa wajumbe kusisitiza uwekezaji kwenye eneo la utafiti na
ubunifu kama chachu ya nchi maskini kupiga hatua za maendeleo.
Dk.
Nungu alisema awali walianza kujadili na kuangalia mifumo katika uwekezaji wa mifumo ya utafiti
na ubunifu ili kutoa matokeo chanya kwa wananchi na nchi zao.
“Niseme
mkutano huu mkuu wa mwaka umekuwa na mafanikio makubnwa sana kwa washiriki hasa
Tanzania kama muandaaji kwani mjadala ulilenga tunachokisimamia,” alisema.
Alisema
wajumbe walishauri utafiti ufanyike kwa mahitaji ya nchi husika na sio kufuata
matakwa ya wafadhili jambo ambalo Tanzania wanalitekeleza kwa asilimia kubwa.
Mkurugenzi
huyo wa COSTECH alisema Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya utafiti na
ubunifu hivyo tume itahakikisha utafiti unaofanyika unakuwa na matokeo chanya
yaonekane.
“Mwananchi
wa kawaida anatakiwa kuona malengo ya utafiti un aofanyika na ili kuona matokeo
ni lazima kuzingatia misingi ya utafiti hasa katika eneo la sayansi wazi,”
alisema.
Aidha,
alisema katika kuhakikisha utafiti unaofanyika unakuwa na tija wamekuwa
wakishirikisha nchi zilizoendelea ili kuona kama zinakuwa na uwiano.
Dk.
Nungu alisema iwapo utafiti utakuwa wa wazi na shirikishi utasaidia watafiti
hasa wa nchi jirani kushirikiana kwa kupeana taarifa bila kufichana.
Alisema
pia watafiti wanapaswa kushirikiana hasa katika eneo la miundombinu kama
maabara ambazo kwa nchi za Afrika hazipo.
Dk.
Nungu alisema iwapo utafiti unaofanywa na watafiti watapewa kipaumbele ni wazi
kuwa maendeleo ya nchi husika yatapatikana.
No comments:
Post a Comment