Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) Dk. Ellen Otaru.
Na Happiness Mnale
IMEELEZWA kwamba ndani ya saa moja jua linaweza kutoa nishati inayoweza kutumika mwaka kwa mwaka mmoja.
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari za Mazingira (JET),
Dk. Ellen alisema tunapotumia nishati jadidifu ikiwemo umeme wa jua ni vyema kuwahamasisha Watanzania kuhakikisha inakuwa salama kwao na rafiki wa mazingira.
Dk. Ellen alisema, kwa kutengeneza paneli za sola ni vyema kuangalia upande wa pili, ni madhara gani anapata Mtanzania kwa miaka mitatu,mitano.
“Hatusemi wasitumie bali tuwaelimishe matumizi sahihi,”alisema.
Mkufunzi kutoka Nukta Africa, Mkurugenzi Mtendaji, Nuzulack Dausen, akifundisha kuhusu uandishi wa takwimu, alisema kupata data ni jambo na kung’amua ni stori iliyojificha kwenye Data ni jambo jingine.
Mafunzo hayo yanafadhiliwa na Shirika lisilo la kiserikali Hivos, Nukta Africa na Chama cha waandishi wa Habari za Mazingira (JET).
No comments:
Post a Comment