HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 26, 2019

LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019 KUWAKUTANISHA WADAU WA UTALII MKOANI KAGERA

Na Lydia Lugakila, Kagera

Kongamano, Bonanza na Maonesho ya Utalii yenye lengo la kukuza mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii linatarajia kuwakutanisha  wadau wa sekta ya hiyo kuanzia Desemba 27 hadi 30 mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Lake Victoria Basin Tourism Expo, Anic Kashasha (pichani), amesema malengo ya kampuni hiyo katika kufanya kongamano Bonanza na maonesho hayo ni kujadili kwa pamoja na wadau wa sekta ya Utalii katika kuona namna ya kukuza mnyororo wa thamani katika sekta hiyo.

Amesema kongamano hilo limefikia katika hatua nzuri na litafanyika kati ya Desemba 27 hadi 30 mwaka huu.

Kashasha amesema kuwa juhudi za kuupandisha uchumi wa Kagera na Tanzania kwa ujumla zinahitajika  hivyo kongamano na maonyesho hayo yataleta tija kwa wadau wa sekta hiyo nje na ndani ya mkoa wa Kagera.

Mkurugenzi huyo amesema mkoa wa Kagera una fulsa na vivutio vingi na kuwa vivutio hivyo havitakiwi kuonekana tu bila faida kwa wananchi wake badala yake vitumike katika kuleta manufaa kwa wanakagera na Watanzania wote kwa ujumla.

Aidha amewaomba wadau mbali mbali wa sekta hiyo nje na ndani ya mkoa wa Kagera kuudhulia kwa wingi katika kongamano hilo ili waweze kupata uelewa wa pamoja katika kuinua kipato cha mwananchi mmoja moja  na Taifa kwa ujumla huku akimpongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa za kupambana na kukuza uchumi katika kufungua milango ya sekta ya Utalii nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba mkoani Kagera, Sabin Bakari, ambaye pia ni mdau katika kongamano hilo amesema Benki hiyo itashiriki kikamilifu katika masuala ya utalii na kuongeza kuwa atahakikisha inapatikana mikopo inayowezesha watalii  katika kukamilisha dhamila yao.

No comments:

Post a Comment

Pages