HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 11, 2019

MPC yaadhimisha nusu karne kuanzishwa kwake

 Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya tangu kuanzishwa kwake Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC). Kulia ni Mratibu wa MPC,
Rose Mwanga. 
(Na Mpiga Picha Wetu).
 Wenyeviti wastaafu wa MPC, Abubakar Karsan, Jimmy Luhende na Osoro Nyawangah, wakipokea vyeti.



Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeonya waandishi wa habari wanaomiliki Televisheni za mkondoni (Online TV), ikisema itaanza kumkamata mmoja baada ya mwingine.


Onyo hilo limetolewa na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, alipozungumza kwenye maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC).


Sherehe hizo zimefanyika jijini Mwanza leo, siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"Kwa Mkoa wa Mwanza peke yake wapo watu 12 wanaomiliki Online TV bila kusajiriwa. Kwa Kanda ya Ziwa wapo zaidi ya watu 60.

"Tunawajua kwa majina na namba zao za simu. Tulishawaita tukawaonya. Mtu unamuona anatulia siku mbili tatu, halafu anaibuka tena. Nawaambia tutawakamata," Mihayo amesema.

"Kuendesha Online TV bila kusajiliwa, unafanya makosa ya mtandaoni. Sheria yetu TCRA inatulazimisha kuwakamata," Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa amesisitiza.


    KUHUSU MPC

Mihayo ameeleza kufurahishwa na uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani hapa, unavyotekeleza majukumu yake katika kuchochea maendeleo ya kisekta.
 
Amesema ushirikiano ulioimarishwa na MPC dhidi ya wadau wa maendeleo ni kielelezo cha mafanikio, hivyo wanahabari wote wanapaswa kufanyakazi kwa kuzingatia sheria za nchi.

  "Mmeniambia leo hapa mna mradi wa kujenga jengo lenu la kitega uchumi la gorofa tatu. Nawapongezeni sana.

"Lakini, mnaweza kuanza na ujenzi wa jengo dogo la kawaida mkaanza kuingiza mapato," amesema Meneje huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa.


Kuhusu uanzishwaji Mradi wa Kituo cha Mawasiliano (Telecenter), Mihayo ameomba uongozi wa klabu hiyo ya wanahabari mkoani Mwanza kuuharakisha zaidi.


"Nina mwaka mmoja hivi tangu nihamie hapa Mwanza. Nimejifunza mambo mengi mazuri kutoka Mwanza Press Club na washirika wake. Naomba tuendelee kushirikiana," Mihayo amekaririwa.


Edwin Soko, Mwenyekiti wa MPC mbali na kuhimiza mshikamano baina ya wanachama na wadau, ameshauri wanahabari kujitenga na uhalifu wa kimtandao.


Kwa mujibu wa Soko anayehudumu pia katika jukwaa la utetezi wa haki za kibinadamu, amesema sheria ya makosa ya mtandaoni isipoepukwa itawaumiza watu wengi.


"Ukiwa mwandishi wa habari au mtu mwingine yeyote, hakikisha unapofanya kazi zako zingatia sheria. Tunazo sheria kali zinazostahili pia kufanyiwa marekebisho.


"MPC tunaendelea kujiimarisha maradufu kiutendaji na ubunifu wa miradi. Kwa sasa tuna kiwanja tunataka kujenga jengo la gorofa tatu. Tupo mbioni pia kuanzisha Online TV," amekaririwa Soko.
 

Amewapongeza wenyeviti waliowahi kuhudumu MPC, akiwamo kiongozi wa kwanza John Kaswezi, Abubakar Karsan, Jimmy Luhende, Deus Bugaywa na Osoro Nyawangah.  

Amesema viongozi hao kila mmoja aliitumikia taasisi hiyo ya kihabari kwa namna yake, hivyo wanastahili sifa na kuwa washauri wazuri.

Mwenyekiti mstafu wa MPC, Karsan ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) ameuambia ulimwengu kuwa:
"UTPC tumekuja na mradi wa kuhakikisha kila klabu ya waandishi wa habari nchi nzima zinaanza kumiliki Online TV."

MPC ilisajiriwa rasmi Disemba 9,1994, ambapo jana imehitimisha miaka 25 ambayo ni nusu karne, ikiwa ni Klabu ya Waandishi wa Habari ya kwanza kuasisiwa

No comments:

Post a Comment

Pages