NA FARAJA EZRA
JUKWAA
la wafanyabiashara kutoka Sekta binafsi (TPSF) kwa kushirikiana na
Serikali wamezindua mfumo mpya wa Kielekroniki (NFLIP) utakaosaidia
kuwapunguzia gharama za usafirishaji wa mizigo inayotoka na kuingia
nchini.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Miradi ya Uendeshaji wa Biashara nchini Edward Furaha,
alisema mfumo huo utarahisisha Usafirishaji wa mizigo kutoka sehemu
moja kwenda nyingine.
Aidha
Furaha alisema Mfumo huo unaitwa 'National Freight Logistics
Informations Portal' (NFLIP) na utakuwa mahususi kuratibu mchakato wa
usafirishaji wa mizigo.
Alisema
mfumo huo awali wasafirishaji walikuwa wakisafirisha mizigo kwa muda
mrefu na madereva walikuwa wakipata usumbufu hasa katika bandari sehemu
ya mawasiliano kati ya mfanyabiashara na mnunuaji mzigo, hivyo mzigo
kukaa kwa muda mrefu bandarini.
Furaha
alisema Tanzania ni Nchi pekee iliyozungukwa na Nchi 6 zisizokuwa na
Bandari hivyo kuzinduliwa kwa Mfumo huo utasaidia kuwavutia Wawekezaji,
Wafanyabiashara waliokuwa wakitumia bandari na jambo ambalo litasaidia
kuongezeka kwa pato la Taifa.
Alifafanua
kuwa mfumo huo utarahisisha kupunguza gharama katika soko zima la
usafirishaji mizigo na Utatumika nchi nzima na kwa upande wa
wasafirishaji kutoka nje unapatikana mtandaoni.
Naye
Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba Group Azim Dewji, alisema licha ya
changamoto wanazopitia wafanyabiashara bado wanaendelea kuishukuru
serikali kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu
ikiwemo viwanja vya ndege, Bandari, Reli, na barabara.
Aidha
Dewji alisema hiyo ni ishara ya kuona kuwa serikali ina mapenzi mema
na ya kuwasaidia wananchi wake lengo likiwa kukuza nankuinua uchumi wa
viwanda.
Pia amewataka
madereva wanaosafirisha mizigo nje ya nchi kuwa mabalozi wema
wanapofanya mawasiliano kwani wamebeba utambulisho wa taifa la Tanzania.
"Madereva
wengi wanapojitambulisha mara nyingi wanatoa kauli ambayo haina staha
kwa jamii husika hivyo tunatafsiriwa kwa mtazamo hasi, ndiyo maana
nimetoa msisisizo kuwa wawe mabalozi wema," alisema Dewji.
Alisema
sekta binafsi ikishirikiana vema na serikali katika kuimarisha
miundombinu ya usafirishaji hakika uchumi wa kati unapatikana kwa
urahisi.
No comments:
Post a Comment