HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 28, 2019

UHAKIKA WA MAJI UNATOKANA NA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI BONDE LA WAMI/RUVU

 Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akizungumza na wanajumuiya watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) wakati wa ziara wa Jumuiya ya Bonde la Wami/Ruvu kutembelea namna ya utunzji wa vyanzo vya maji katika msitu wa Amani wilayani Muheza mkoani Tanga.
 Afisa Udhibiti  Ubora wa Huduma  na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka akitoa maelezo kuhusiana na namna walivyonufaika Mamlaka hiyo  kutokana na jamiI kuwa na uthubutu wa kuhifadhi vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku akizungumza kuhusiana na umoja huo walivyopokea utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja kuinuka kiuchumi wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu.
 Mwenyekiti wa Makinga Maji Mkazi wa Kijiji cha Mbomole  Michael Simon akieleza kwa waandishi wa  habari namna ya makinga maji yanavyosaidia katika kuhifadhi vyanzo vya maji pasipo kuwepo kwa udongo wa kutiririka ka vyanzo vya maji.
 Maji yakitiririka msimu mzima wa mwaka  katika Msitu wa Amani wilayani Muheza.
 Mmoja wa wenye viti wa Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Basley Matangaru akieleza namna walivyopata elimu  ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji  katika umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI.
 Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI wamejenga sehemu mahsusi kwa ajili ya kuonyeshea pikipiki ili wasiweze kutiririsha uchafu katika vyanzo vya maji.
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akimkabidhi fedha taslimu sh.100,000 kwa Katibu Msaidizi wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI Willium Masonda kwa ajili ya uhamasishaji wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kikundi cha hamasa vhs umoja huo.

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii  Amani, Tanga
Katika kuendelea kuwepo kwa maji ya uhakika na yenye usalama hakuna budi jamii kuhifadhi vyanzo vya maji wanavyozunguka kwa kuendesha shughuli za kilimo zisizo na madhara katika vyanzo hivyo.
Vyanzo ya maji vikihifadhiwa kwa katika sekta ya kilimo kwa kupanda mazao ambayo hayana madhara katika utiririshaji maji mamlaka husika kupunguza gharama za kutibu maji wakati wa usambazaji wa maji hayo kwa wananchi.
Mkoa wa Tanga kwa wananchi wanaozunguka vyanzo vya maji wameunda Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira  Kihuhwizigi (Uwamasiki) ambao wamekuwa wakihifadhi vyanzo vya maji na kufanya mamlaka  ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga Tanga Uwasa) kuunga mkono jitithada za umoja huo.
Kutokana na Mamlaka ya Tanga kuwa umoja wenye nguvu katika uhifadhi vyanzo vya maji Bonde la  Wami/Ruvu imepeleka jumuiya za Watumia Maji katika vyanzo vya bonde hilo kujifanza katika umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Uwamasiki) ili kuleta chachu kuongeza mbinu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza  amesema kuwa wamepeleka jumuiya hizo kwenda Tanga kwenda kujifunza namna Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Kihuhwi) inavyolinda vyanzo vya maji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo hivyo ikiwemo kilimo.
Kayoza amesema baada ya kutoka Tanga nia ni kuona jumuiya ya watumia maji wanakwenda na kasi ya  kuweka mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kushirikisha wadau wote kwa kutumia elimu walioipata katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
Aidha amesema kuwa mazingira ya vynzo vya maji katika mkoa wa Tanga havina tofauti na Mikoa ya Morogoro na  Pwani hivyo wanajumuiya ya watumiaji katika Bonde la Wami/Ruvu watatumia mbinu mbalimbali walizozipata katika ziara ya Tanga.
Nae Afisa Udhibiti  Ubora wa Huduma  na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka amesema kuwa kutokana na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) kuhifadhi vyanzo vya maji kumeleta matokeo chanya kwa mamlaka kupunguza gharama za kutibu maji.
Amesema kuwa wakati umoja huo ukiwa haujaanzishwa walikuwa wanatumia gharama kubwa ya kutibu maji lakini kuanzishwa kwa umoja huo Tanga-Uwasa limeendelea kupunguza gharama hizo ikiwa ni kuunga mkono kwa ufadhili wa miradi kwenye umoja ili waendelee kutunza vyanzo vya maji.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku amesema kuwa umoja umesimama vizuri kutokana na kila mmoja kujua umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji.
Amesema wakati wanaanza umoja huo kuna vyanzo vingine vilikuwa vimekufa lakini sasa vyanzo vyote vinatiririsha maji wakati wote  huku shughuli za kiuchumi zikiendelea bila kuathiri vyanzo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages