HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2019

VIONGOZI WATAKIWA KUTUMIA BUSARA ZA MWALIMU NYERERE: DKT. BASHIRU

Na Lydia Lugakila, Kagera

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliopo katika nafasi za uteuzi nchini wametakiwa kutumia Busara za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili zile pilikapilika za kutafuta uongozi zisikidhoofishe chama  hicho.

Kauli hiyo  imetolewa na Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Dkt Bashiru Ally wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa chama uliopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Dkt Bashiru amesema viongozi wanapaswa kuenenda katika mifano mizuri ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo ameeleza kuwa miaka 60 ya Mwalimu Nyerere Mwalimu  aliamua kuachana na  uwaziri mkuu na nafasi hiyo kumwachia Mzee kawawa ili yeye afanye kazi moja ya kuimalisha  misingi ya chama cha Tanu.

Amesema baadaye Mwalimu Nyerere alirudi kwenye dola baada ya kujilidhisha kuwa chama cha Tanu kikao imara.

Dkt Bashiru amesema kuwa Mwalimu Nyerere aliamini kabisa kuwa chama legelege huzaa serikali legelege na baadae alisema bila CCM madhubuti nchi hii itayumba.

"Sasa nyie viongozi wenzangu tulioko kwenye chama  mlioteuliwa kama mimi na nyie mliomba kura 2017 kwanini mnataka kukimbia nafasi za kuimalisha chama Kipi kizito zaidi? aliuliza Katibu huyo.

Amesema viongozi hao wanapaswa kutumia busara ya Mwalimu Nyerere ya miaka 60 na kuwa hali ni haki na kuna busara yake pia.

Amesema wapo baadhi ya viongozi wakati wa kugombea hupalamia fomu na kuzunguka zunguka kwa kutamka neno mnione, mnione.

Ameongeza kuwa viongozi wanatakiwa kuacha misuko suko ndani ya chama badala yake waimalishe misingi ya chama kwa kufuata taratibu zote za chama hicho.

Dkt Bashiru amesema msimamo wake uko pale pale wa kutumia busara ya Mwalimu hasa kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuimalisha chama ili chama kitafute dola.

Akiendelea kuelezea  busara ya Mwalimu ya mwaka 1985 aliponga'tuka Urais ilikuwa si uamuzi wa kawaida katika nchi kwani wananchi hawakuwa na uhakika kama kuna Mbadala wake lakini kwa busara zake akawaeleza kuwa "yeye si Mungu wala hana miujiza ya Mwenyezi Mungu bali kuna ukomo wa vipaji vyake na  kuna ukomo wa uwezo wake.

"Mwalimu Nyerere alisema Nang'tuka naachia dola hapo ndipo Busara ilipotumika ili ajipange vizuri kwa mazoea mapya ya Tanzania bila Mwalimu Nyerere.

Pia katibu huyo ameeleza kuwa mwaka 1985 hadi mwaka 1990 Mwalimu ameendelea kuwa mwenyekiti wa chama kwa ajili ya kuimalisha chama na ukawepo mpango wa kuimalisha chama ambapo alizunguka nchi nzima akaacha dola akaimalisha chama.

kutokana na maelezo hayo ya Dkt.  Bashiru akapata swali la kuwauliza viongozi hao" Sasa je wangapi wako tayari kuachia dola na kwenda kuimalisha misingi ya chama.

Wakati jibu likiwa bado halijapatikana kwa viongozi hao akawahimiza wanachama hao hasa wale ambao kanuni inawataka wawe na nafasi moja kwa wakati mmoja na wala sio nafasi mbili kwa wakati mmoja wakati wa uchaguzi kuacha tabia ya kupoteana, kuchanganyana kwa visingizio vya neno:- Haki yangu Mimi Kugombea na kuchaguliwa.

Hata hivyo ameongeza kuwa kila penye haki pana wajibu hivyo viongozi wa chama wana wajibu wa kuhakikisha kwamba chama kinashia kinashika dola bila kuanza kukimbia viti jambo linalosababisha kupoteana na kusababisha mpasuko katika chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Pages