HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2019

NIYONZIMA KUTUA DAR LEO

Haruna Niyonzima.  
 
Na John Marwa

Kiungo fundi Haruna Niyonzima anatarajiwa kuwasili nchini leo kujiunga na Yanga tayari kwa maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba Januari 04 2020.

Niyonzima anayerejea Yanga kwa mara ya pili, ameandaliwa mapokezi makubwa ambapo mashabiki watapewa nafasi ya kumpokea nyota huyo mwenye heshima kubwa katika klabu ya Yanga

Niyonzima huenda akatambulishwa kesho kabla ya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Biashara United ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Habari njema ni kuwa baada ya kumsajili tu Yanga ilianza mchakato wa kufuatilia vibali vyake na hivyo ataweza kushiriki mchezo wa Januari 04

 Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kujiamini na watembee kifua mbele kwani timu yao sasa iko katika hali nzuri baada ya baadhi ya changamoto kumalizwa

Wiki chache zilizopita, Yanga ilikuwa na changamoto ya kulipa mishahara ya wachezaji hali iliyopelekea baadhi ya nyota kuomba kuvunja mikataba yao

Nugaz amesema suala hilo litabaki kuwa historia baada ya wadhamini wao GSM, Taifa Gas na Sportpesa kuwapa sapoti ya kulimaliza

"Nawaambia mashabiki wa Yanga watembee kifua mbele, wasiyumbishwe na yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii na wapinzani wetu kwani sasa mambo ni mazuri"

"Hatuna changamoto ya kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na stahiki nyingine. Wadhamini wetu GSM, Taifa Gas na SportPesa wametuhakikishia kuwa suala la kulipa mishahara ya wachezaji halitakuwa tatizo tena"

"Tena wakae mkao wa kula kuwapokea nyota watatu ambao tumekamilisha usajili wao. Tembeeni kifua mbele kwani matatizo yamekwisha Yanga," alitamba Nugaz.

No comments:

Post a Comment

Pages