HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 21, 2019

WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA MTUMBWI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ACP Revocatus Malimi.



Na Lydia Lugakila, Kagera

Chanzo cha watu watatu kufariki dunia wilayani Ngara mkoani Kagera chatajwa huku watoto wawili akiwemo  mwanafunzi wa darasa la tatu  wilayani Muleba mkoani Kagera kupoteza maisha baada ya mtumbwi walokuwa wakiutumia kupinduka katika katika ziwa Victoria.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vifo hivyo vya watu watano katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilaya ya Ngara na Muleba mkoani Kagera, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amesema katika tukio la kwanza lililotokea katika kijiji cha Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera limewataja watu watatu ambao ni Sinzu Musi Jerard, Minani Ramadhani na Mwambazi Sevelin wote raia wa nchi ya Burundi waliokuwa wakifanya shughuli za kuchimba madini  wamefariki ndani ya shimo baada ya kukosa hewa safi huku chanzo nikiwa ni katika hali ya kutii masharti ya mganga wao yaliyolenga kuwapatia Mali zaidi ndani ya mgodi huo.

Kamanda Malimi amesema kuwa watu hao wamepoteza maisha baada ya kuingia kwenye mgodi huo kwa Masharti waliyopewa na mtaalamu wao kwa maana ya mganga ya kufukiza au kuchoma moto ili waweze kupata Mali nyingi ndipo walifanya kitendo hicho cha kuchoma dawa hiyo wakiwa ndani ya shimo la mgodi wenye urefu wa mita 35 na kusababisha kukosa nguvu kutokana na hewa safi kupungua.

Aidha kamanda Malimi amesema katika tukio la pili watu wawili waliokuwa wakifanya shughuli za Uvuvi katika ziwa Victoria eneo la Ilemela wilayani Muleba mkoani hapa ambao ni Robson Jovinary mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiga na Christian Paulo wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kupinduka wakati wakivua samaki.

No comments:

Post a Comment

Pages