Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kubadilishana uzoefu wa masuala ya itifaki baina ya Tanzania na ZImbabwe. Mhe. Zindoga amekuja nchini kujifunza jinsi gani Tanzania inaratibu masuala ya kiitifaki kufuatia kufanikisha kwa mafanikio makubwa ya mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika mwezi Agosti, 2019 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga akimueleza jambo Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati walipokutana na kufanya mazungumzo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Chipo Zindoga wakati wa mazungumzo baina yao jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Itifaki na Kitengo cha Utafiti, Ofisi ya Rais, Zimbabwe Mhe. Balozi Chipo Zindoga mara baada ya kukamaliza mazungumzo yao mazungumzo yao.
No comments:
Post a Comment