HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 28, 2020

BARAZA LA MANISPAA YA TABORA LAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA BILIONI 69 KWA AJILI YA MWAKA UJAO WA FEDHA

NA TIGANYA   VINCENT, TABORA
 
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 69.5 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha wa 2020/2. 

Madiwani hao wamefikia hatua hiyo jana mara baada ya Mchumi wa Manispaa ya Tabora Joseph Kashushura kuwasilisha mapendekezo hayo na Madiwani kwa pamoja wakaunga mkono mapendekezo.

Akichambua mapendekezo hayo, Kashushura alisema  mapato ya ndani ya Halmashauri wana lengo la kukusanya shilingi bilioni 4.8 sawa na ongezeko la asilimia 4 ukilinganisha na masikio ya mwaka 2019/20wa bilioni 4.6 kutoka vyanzo vya ndani.

Kashushura alisema kutoka Serikali Kuu  wanatarajia kupata jumla shilingi bilioni 64.7 ikiwa ni ongezeko la asilimia 69 ukilinganisha na bilioni 38.2 ya mwaka 2019/20.

Alivitaja vipaumbele katika bajeti ijayo kuwa ni uendelezaji wa jengo la utawala ambalo limetengewa milioni 200 , kuwa na fedha za ununuzi wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji milioni 80 , imetenga milioni 25 za ununuzi wa hekta 107 kwa ajili kupima maeneo ya ujenzi wa Taasisi mbalimbali kama vile za afya na elimu.

Kashushura alisema vipaumbele vingine ni kutenga milioni 145 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule katika Kata mbalimbali na kiasi cha milioni 50 za ulipaji fidia kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi.
mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages