Na Robertha Makinda - BRELA
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Godfrey Nyaisa, amewasili rasmi katika kituo chake kipya cha kazi leo
Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili katika BRELA Ofisi Kuu Bw. Nyaisa amepata wasaa kukaa kikao kifupi na Menejimenti, kutambulishwa kwa wafanyakazi pia kukutana na baadhi ya wadau wa BRELA waliokua wakipata huduma kwa siku ya leo.
Katika maneno yake ya utambulisho kwa wafanyakazi wa BRELA amewataka wampe ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii.

“Wafanyakazi wanzangu naomba kwa kipindi hiki tushirikiane ili tuweze kufanya kazi za serikali ni matumaini yangu kila mmoja atasimama katika nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma ya Tanzania ya Viwanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati”, alisema Bw. Nyaisa.
Aidha alipokua akizungumza na wadau wa BRELA waliokuwa wakipata huduma siku ya leo, amewaomba waweze kuwa wavumilivu kwa kwa kipindi hiki wakati BRELA inajipanga kutoa huduma bora na kuondoa malalamiko yaliyopo, alibainisha Bw. Nyaisa.
Bw. Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020 akichukua nafasi ya Bi. Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.
Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana wadau wa BRELA
alipokua akitembelea Ofisi za Idara na Vitengo mbalimbali baada ya
kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es
Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.
Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara
ya Leseni BRELA Bw. Andrew Mkapa mara baada ya kuwasili leo Januari 23,
2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Huduma na Uwezeshaji Bw. Bakari Mketo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.
Godfrey Nyaisa (Mbele) Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo
Mbalimbali BRELA mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi
Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment