NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa wilaya ya Tabora Komanya
Kitwala ametoa siku saba kwa Afisa Mazingia wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha
ameweka vibao vinavyozuia utupaji wa takataka katika maeneo ambayo sio rasmi
ili sehemu ya kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Alisema
kutokewepo kwa vibao hivyo kumesababisha baadhi ya watu kutupa taka
hata katika maeneo ambao sio rasmi na kusababisha kuzagaa kwa taka na
kuhatarisha afya za wananchi.
Kitwala ametoa kauli hiyo juzi wakati
wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora cha kupitia mapendekezo ya
bajeti ya mwaka 2020/21.
Alisema baada ya kuweka vibao ni vema
wakaweka Askari wa Jeshi la Akiba ambao hawana sare kuwavizia wale wote
wanaokaidi agizo la kutotupa taka ovyo na kuwakamata ili watonzwe fedha kulingana
na maagizo ya Sheria ndogo ndogo za Halmashauri.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliuagiza
uongozi wa Manispaa ya Tabora sehemu ya mazingira kuhakikisha wanaongeza vifaa
vya kuweka taka katika maeneo mbalimbali ya Manisapa ya Tabora ili kuondoa visingizio kwa baadhi ya
watu wanaotupa taka ovyo kwa madai hakuna vifaa vya kuwka taka mitaani.
Kwa upande wa Mazingira wa Manispaa
ya Tabora William Mpangala alisema zoezi la kuandaa vibao vya matangazo ya
kupiga marufuku utupaji wa taka katika maeneo yasiyo rasmi limeshaanza na
wanatarajia ndani ya mwezi huu kuvisambaza katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment