HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2020

KANISA LA ABC JIJINI DAR ES SALAAM LAPATA MAFUNZO YA KUSAIDIA JAMII KUTOKA MAREKANI

 Vijana wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata Mandela jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mandela wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kwenda kutoa msaada kwa waathirika 20 wa mafuriko na wazee wasiojiweza wanaoishi mtaa huo. Kulia ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya ABC, Flaston Ndabila. Msaada huo waliutoa wakati wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ya kusaidia jamii yanayotolewa na muumini wa kanisa hilo Tamari Mwakakonyole Shunda anayeishi Marekani. 
Vijana hao wakielekea kutoa msaada huo.
Msaada ukitolewa.


Na Dotto Mwaibale
VIJANA wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC) la Tabata jijini Dar es Salaam wameanza kupata mafunzo ya kusaidia jamii, Afya, kujizuia kupata madhara yatokanayo na majanga.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana walio ndani ya Community Health Workers (CHW) iliyoanzishwa  kwa kushauriwa na muumini wa kanisa hilo Tamari Mwakakonyole Shunda ambaye anaishi Marekani.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Tamari Shunda akizungumza kwa njia ya mtandao alisema Community Health Worker ni somo la muhimu kuwafundisha watu hasa vijana wanaopenda kujifunza.
"Napenda kufundisha somo hilo la CHW kwani pamoja na kuwasaidia watu kuelewa, dalili na hasa ni nini kinachofanya watu waumwe magonjwa mbali mbali na namna ya kujizuia walengwa sio kwa  hao vijana na wanafunzi pekee bali ni ndugu, jamii zao  majirani na hata sehemu wanapo abudu.
Alisema Kanisa la ABC chini ya uongozi wa Askofu Flaston Ndabila  baada ya kuwapa ushauri wameonesha hamu ya kujifunza na tulichoweza kukifanya ni kuwaweka kwenye makundi mawili.
Alisema kundi la   kwanza ni 'Traine the Trainer' , na la pili ni wale wote wanaoweza kujifunza.
Alisema licha ya masomo hayo kutolewa kwa njia ya mtandao wanafunzi hao wameonesha bidii kubwa ya kujifunza jambo linaloleta matumaini. 
Aliongeza kuwa kwa vile CHW  ipo msitari wa mbele katika mambo ya jamii na wanaishi kwenye sehemu wanaotoa huduma, ni wa muhimu sana kwenye society zozote zinazoendelea kwani daktari hawezi kuwa kila sehemu na hata wauguzi hadhani kama wanatosha kuweza kukabiliana na mahitaji ya watu. 
" Mwanzoni mwa mwezi huu tulifanya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi hao ili kuwapa elimu ya kutumikia jamii ambapo walikwenda kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Tabata Mandela na hii iliwaongezea uelewa wa namna ya kukabiliana pale inapotokea dharura na kuwa mstari wa mbele kutoa msaada.
"Mafunzo hayo ya vitendo yameonesha jinsi wanafunzi walivyo yaelewa hasa baada ya kuandika ripoti zao" alisema Shunda.
 Alisema mafunzo hayo ni ya muhimu kwani hata yeye amefanya kazi hiyo ya kujitolea kusaidia jamii huko Marekani kwa zaidi ya miaka kumi ikiwa ni pamoja na kufundisha jinsi ya kujizuia na magonjwa na watu kubadilisha hali na tabia zinazo sababisha madhara kwenye afya zao.
Alisema anapenda kuendelea kufundisha masomo hayo  na wanafunzi watakao hitimu watakabidhiwa vyeti vyao mwezi wa tano mwaka huu na kuwa kwa wale wanaopenda kuendelea kusoma katika taaluma tofauti za afya fursa hiyo ipo.
Shunda alisema nchi yetu inahitaji  wana CHW kwa ajili ya kusaidia  kuyakabiri madhara ya magonjwa kabla hayaja leta hadhari  zaidi na  watu watajifunza kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mwenyekiti wa CHW, Gad Ndabila alisema mafunzo hayo yamewapa uelewa mkubwa na kujifunza mbinu za kusaidia jamii katika masuala ya afya na namna ya kuweza kuzuia kupata madhara na kujikinga.

No comments:

Post a Comment

Pages