HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2020

NZEGA TC KUKUSANYA BILIONI 18 MWAKA UJAO WA FEDHA

NA TIGANYA VINCENT

HALMASHAURI ya Mji Nzega inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 18 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 kutoka vyanzo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magesa wakati wa kikao cha Sekretaieti ya Mkoa wa Tabora cha kuchambua na kujadili mapendekezo ya makisio ya mipango na bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka 2020/21.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha wameweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 2.500 kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Magesa  alisema mapendekezo ya bejeti ijayo imezingatia agizo la utengaji wa asilimia 40 wa fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na asilimia 10 kwa ajili ya mikopo ya wanawake , vijana na walemavu.

Alisema katika mapendekezo ya bajeti ijayoa wanatenga shilingi bilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 32 ya maendeleo inayohusu sekta mbalimbali.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo aliongeza kuwa kwa kuwa mwaka ujao wa fedha wanatarajia kuchukua unendeshaji wa Hospiatali ya Wilaya kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na kuhamia Nzega Mji  wametenga kiasi cha bilioni 1.300 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Hospitali hiyo kuanzia Julai

No comments:

Post a Comment

Pages