Akizungumza katka mgahawa huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif, alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwahamasisha wateja wa Benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. “Pamoja na punguzo la asilimia kumi kwa malipo yao, wateja wetu pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fulana, vikombe na nyingine vingi.
Meneja wa Bar ya Tips Beach Kidimbwi, Bi Joan Pascal, alisema kuwa wateja wao wamefurahia sana kampeni hiyo kwani ni mwanzo mpya wa kuachana na utamaduni wa kutumia fedha taslimu kufanya malipo.
Afisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Francis Mgani (kushoto), akimkabidhi zawadi ya fulana, Patrick Michael, baada ya kufanya malipo kwa kutumia TemboCardvisa wakati wa mwendelezo wa kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu. Kampeni hiyo hiyo ilifanyika katika Mgahawa wa Beach Kidimbwi uliopo Mbezi Beach, jijini
Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Wakala FahariHuduma, Nasra Abdallah (kulia), akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliofika katika Bar ya Beach Kidimbwi.
Mteja akifungua akaunti Mpya ya Benki ya CRDB.
Afisa wa Benki ya CRDB, Bi. Rehema, akimpa zawadi mteja wa benki hiyo baada ya kufungua akaunti Mpya wakati wa mwendelezo wa Kampeni ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu.
Mteja wa Benki ya CRDB, akifanya malipo kwa kutumia TemboCardvisa wakati wa mwendelezo wa kampeni ya ‘Chanja, Lipa, Sepa’ ya kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia kadi na kuachana na mfumo wa kutembea na fedha taslimu, iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Huduma za Uwakala CRDB, Fadhil Mollel.
No comments:
Post a Comment