Mohamedduwaid Abdullathif.
Nawal Shebe.
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Mashindano ya kuogelea ya
Taliss-IST yamepangwa kufanyika kuanzia Februari 22 mpaka 23 kwenye bwawa la
kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki.
Mashindano
haya yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji kutoka klabu zote za Tanzania Bara na
Zanzibar kwa mujibu wa Meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe.
Hadija
alisema kuwa wanatarajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkubwa kutokana na
maandalizi ambayo klabu mbali mbali yameanza kufanya mpaka sasa.
Alisema kuwa
kila mwaka ushindani na ubora wa mashindano yao unaongezeka na kuwavutia
mashabiki wengi mchezo huo wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
“Tumejipanga
vyema kwenye mashindano haya na hasa ukizingatia kuwaklabu nyingi zimepiga
hatua kubwa na kuleta ushindani huku waogeleaji wengi wakisaka medali, vikombe
na vile vile kuhimarisha muda (Pbs),” alisema Hadija.
Waogeleaji watashindana
katika umri tofauti ambao ni chini ya miaka nane, miaka tisa na 10, 11 na 12,
13 na 14. Pia kutakuwa na mashindano ya waogeleaji wenye umri kuanzia zaidi ya miaka
15.
Jumla ya
staili tano za kuogelea zitashindaniwa katika mashindano hayo. Staili hizo ni backstroke,
butterfly, freestyle, breaststroke na Individual Medley.
Waogeleaji pia
watashindana katika relei mbalimbali ambazo zinaleta ushindani mkubwa.
Hadija
alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi watatu wa kwanza katika
kila tukio ambao watapewa medali ya dhahabu, fedha na shaba. Washindi wa jumla
katika kila umri watazawadiwa vikombe.
“Tunaomba
wadhamini mbalimbali wanaotaka kusaidia kufanikisha mashindano haya kujitokeza
na kuinua vipaji kwa waogeleaji na kuleta maendeleo kwa ujumla,” alisema
Hadija.
No comments:
Post a Comment