Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,
Prof. Sospeter Muhongo amepanga kuongoza
harambee ya kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa 13 katika
shule zenye ufungufu jimboni humo.
Katika harambee hiyo Prof. Muhongo
atawashirikisha wanavijiji mbalimbali ili kutimiza lengo la kunusuru hali hiyo
itakayookoa wanafunzi 616 wanaotarajia kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu
katika shule hizo zenye upungufu wa vyumva vya madarasa.
Mbunge Muhongo anataajia kutembelea
shule zote za sekondari zenye upungufu huo na hatimaye kuandaa harambee ya
kuwezesha ujenzi wa vyumba hivyo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wasikose
kujiunga.
“Shule zinafunguliwa Jumatatu, tarehe
6.1.2020, bado tunao upungufu wa vyumba 13 vya Madarasa ya Kidato cha Kwanza
(Form I).
Vyumba 13 hivyo visipopatikana wanafunzi
616 watabaki nyumbani wakisubiri uwepo wa Vyumba vya Madarasa yao,”
alisema Prof. Muhongo hivi karibuni jimboni humo.
.
Ameanza kutembelea shule hizo leo na
kuona kila shule vyumba vilivyopungua.
No comments:
Post a Comment