Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, leo January 21 amepokea
Mchango wa Shehena ya Ndoo 500 za Rangi za nyumba kutoka Kampuni ya
utengenezaji wa rangi za Billion Paint iliyomuunga mkono katika
kuhakikisha madarasa ya wanafunzi Mkoani humo yanakuwa katika Mwonekano
Mzuri na wakupendeza.
RC
Makonda amesema Rangi hizo alizopatiwa zitatumika kupaka madarasa zaidi
ya 381 yanayojengwa na Serikali kwaajili ya Wanafunzi 5,970 ambao
walifaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza lakini wakakabiliwa na
changamoto ya uchache wa vyumba vya madarasa lakini kupitia uongozi
thabiti wa serikali ya awamu ya tano madarasa hayo yapo hatua ya mwisho
kukamilika na kukabidhiwa kabla ya March 28 mwaka huu.
Aidha
RC Makonda amepongeza kiwanda hicho kwa kuamua kurudisha fadhila kwa
wananchi kupitia mchango wa Rangi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zitaenda
kutatua changamoto mbalimbali kwenye miundombinu ya majengo ya
wanafunzi.
Pamoja na hayo
RC Makonda amesema amefurahi kuona Kiwanda hicho kinamilikiwa na Kijana
Mzawa alieamua kuitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza
uchumi wa Viwanda na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 40 kiwandani hapo.
No comments:
Post a Comment