Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Possi, akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti
wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo
Fölsen.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo
Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika
kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin, ambako
ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao
ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo
utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya
Tanzania na watanzania, ususani katika sekta ya Utalii,uwekezaji, afya na
elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele, Umoja wa Tanzania
nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio
nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta
maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.
Pia kwa upande
wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana
pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa
kuitangaza vema Tanzania katika nyanza zote na vivutio vyake katika tufe
la dunia ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.
No comments:
Post a Comment