Na Bryceson Mathias
WAKATI zoezi la kusajili simu
kwa alama za vile liendea ukingoni! Wananchi, Ndugu, na baadhi ya walemavu
wasio na Vidole wameilalamikia Serikali kuu wakihoji changamoto ya walemavu
wasio na vidole, wanasajili namna gani simu kwa alama za vidole?.
Aidha wameonesha wasiwasi wao
kutokana na usajili huu wa ‘Mwendo Kasi’ kwamba, Taifa linaweza likaruhusu
wageni kujipenyeza mpaka chumbani kwa sababu rushwa ikitumika kutafuta fursa
hii adimu, maana hata wasio raia wanaitumia ili kufaidi keki hii.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wenye ndugu wasio na mikono au vidole vya mikono kwa sababu ya maradhi
au madhira tofauti tofauti wamedai, baadhi yao wamefanya kinyume kwa kusajili simu
za walemavu hao kwa kutumia majina na vidole vya ndugu zao isivyo sahihi! Je Serikali
inasemaje?
“Waliosema ukweli wakiomba
kuwasajilia simu zao kupitia majina ya wenye viungo walikataliwa na watendaji! Je
kwa msingi huo watasajilije simu zao au serikali itatoa mwongozo mwingine juu
ya wenye ulemavu huo?”.alihoji mwananchi mmoja ambaye aliomba asitajwe.
Mmoja wa Wakazi alisema,”Nalisaidia
Taifa langu, wageni ambao wana uchu wa fursa za Tanzania za kupata Ardhi,
Makazi, Huduma za Kijamii, Kazi, Ufugaji, Uvuvi, Kilimo na shughuli zingine za
kijamii nchini, wanatumia mwanya huo na wengine wanafanikiwa kupenya”.
Hata hivyo katika Kipindi cha
Mjadala wa Tuongee Magazti 18/01/2020, Mwandishi Mkongwe, Jacton Manyerere,
naye alilalama na kushauri kuwa, Waandishi, Watawala watambue wageni wana uchu
na fursa ya Amani ya Tanzania ambapo mtu unaweza kukaribishwa kula usuhojiwe.
Alisema kuna minong’ono
katika baadhi ya maeneo ya wafugaji na utalii ikiwemo nchini, wapo baadhi ya wageni
wamejipenyeza kuanza kusaka usajili huo wa mwendo kasi kwa udi na uvumba ili
wafaidi matunda hayo akidai watatumia hata rushwa na kufanikiwa ukikosekana
umakini, akisisitiza kuchelewa usajili si kosa la wananchi tu!.
Mbali ya Manyrere, Mwandishi,
Peter Saramba, alisema uwezekano wa kusajili simu kwa wakati (meet target) kwa
siku mbili zilizobakia itakuwa ni ndoto, ila anaamini Serikali na Rais John Magufuli
kupitia kwa washauri wake, atakuwa ameona changamoto hiyo, hivyo huenda
akaongeza muda kukidhi changamoto hata za walemavu wasio na vidole na mikono.
No comments:
Post a Comment