NA KENNETH NGELESI, CHUNYA
MKUU
wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameagiza
kupitiwa upya tozo za kuhifadhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya
Chunya.
Agizo hilo
alilitoa katika warsha iliyoandaliwa Baraza la Kikristo Tanzania (CCT)
kupitia mradi wa PETS unaojumisha wananchi ngazi ya Kijiji na Kata.
Mratibu
wa warsha hiyo Edward Mwasote alisema lengo la warsha huyo ni
kuwakutanisha wananchi na viongozi ili kuwasilisha kero zao na serikali
kuzipatia ufumbuzi.
Kwa
upande wake Mwezeshaji wa warsha hiyo kutoka CCT Dodoma Wakili Msomi
Beatrice Tengeneza alisema warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha
wananchi kukutana na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasilisha
kero na mafanikio yaliyofanywa na serikali.
Aidha alisema si lazima kupokea kero tu bali hata mafanikio yaliyofanywa na serikali kwa lengo la kuyafikia maendeleo ya pamoja.
Akiwasilisha
kero mbalimbali kwa niaba ya wananchi Padre Goodluck Mlelwa alisema
hospitali ya Wilaya ya Chunya imekuwa ikitoza tozo kubwa kwa ajilu ya
kuhifadhi maiti kwa siku ambapo hutozwa shilingi elfu arobaini kwa siku.
Mlelwa alisema pia tozo kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza licha ya kuwa na kadi ya bima ya afya.
Naye
Wakili Beatrice Tengeneza kwa niaba ya wajumbe alisema wananchi wa
Kijiji cha Igodima wamelalamikia ubovu wa barabara pia kutokuwepo
huduma za umeme.
Alisema pia kuchelewa kukamilika kwa zahanati kunazorotesha maendeleo.
Akijibu
kero za wananchi kuhusiana na tozo kubwa za kuhifadhi maiti Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Mhandisi Maryprisca Mahundi alimwagiza Mganga Mkuu
Felister Kisandu kuhakikisha wanarekebisha bei hizo kwana chumba hicho
cha kuhifadhia maiti kimejengwa na wananchi.
Mahundi
alisema wananchi wanapaswa kupata huduma kwa gharama nafuu kuliko awali
ambapo wananchi walikuwa wanahidhi maiti Mbeya umbali wa kilometa
sabini na mbili.
No comments:
Post a Comment