HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 23, 2020

WAZIRI DK. HUSSEIN MWINYI KUMALIZA MGOGORO WA WANANCHI NA KAMBI YA KABOYA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Alhaji Dk. Hussein Mwinyi.

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Alhaji Dk. Hussein Mwinyi, yupo mkoani Kagera kwa ajili ya kutatua changamoto  iliyopo kati ya Kambi ya Jeshi ya Kaboya na wananchi.

Akiwa katika ofisi za mkoa wa Kagera kabla ya ziara yake ya kikazi ya kutembelea kambi zenye changamoto ikiwemo ya Kaboya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera Waziri Mwinyi ameahidi kupambana na changamoto ya kutoelewana kati ya kambi hiyo na wananchi.

Akizungumzia changamoto ya kutokuwepo kwa maelewano mazuri kati ya wananchi na kambi hiyo Waziri Mwinyi amesema kuna baadhi ya kambi zimekuwa na changamoto na wananchi ambapo kufika kwake mkoani hapa ni baada ya kupokea taarifa tangu mwaka 2014 ilipoamliwa wananchi walioko ndani ya eneo la kambi hiyo walipwe fidia na wapishe eneo hilo ili jeshi liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi

Waziri Mwinyi amesema kutokana na suala hilo la muda mrefu sasa ameamua kufika ili kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ili suala la maelewano liwepo ambapo amesema kwa makubaliano yaliyofanyika 2014 yalijumuisha mipaka kurekebisha.

"wananchi waliokuwa ndani wakati ule wamebaki nje na wachache waliobaki  hivyo hatuna budi kuwatafutia fidia kuwalipa na kuwatafutia maeneo mengine ili wakaanzishe makazi mapya lengo tumalize tofauti zilizopo alisema "waziri huyo wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.

Waziri Mwinyi amemshukuru mkuu wa mkoa wa Kagera Bligedia jenerali Marco Elisha Gaguti kwa juhudi kubwa za kuhakikisha mkoa unakuwa salama.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemuomba waziri Hussein Mwinyi kuongeza ulinzi katika ziwa Victoria.

Akijibu ombi hilo waziri huyo amemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa tayari suala hilo limeanza kufanyiwa kazi ambapo kiteule chao kitakachoku kigogo feli kilichopo Mkoani Mwanza kitaongezewa uwezo ili kutoa ulinzi wa kutosha katika ziwa victoria.

Hata hivyo Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha mkoa unakuwa salama.

No comments:

Post a Comment

Pages