Na Mwandishi Wetu
Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Bw. Loata Erasto Olesanare amesema maambukizi ya virusi vya UKIMWI
katika Mkoa huo vimeongezeka kwa Kiwango cha 4.2% kwa takwimu za mwaka 2016/12
tofauti na takwimu za mwaka 2011/12 ambapo maambukizi hayo yalikuwa 3.3% na
kuonya kuwa uenda takwimu hizo zikaendelea kama hatua anwai hazitaendelea
kuchukuliwa.
Mkuu huyo wa Mkoa
amesema hayo mapema leo Ofisini yake alipokutana na ujumbe wa Wizara ya Afya
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii uliofika ofisini kwake kwa lengo la kutoa taarifa
ya kampeini ya kumpambana na maambukizi ya UKIMWI kwa vijana ijulikanayo kama
Timiza malengo ili kufikia ndoto zako.
Aidha Bw. Olesanare
ameongeza kuwa kwa takwimu za kila Wilaya katika Mkoa wa wake Kilombero
inaongoza kwa maambukizi ya UKIMWI kwani Wilaya hiyo kwa takwimu za mwaka
2016/17 maambukizi katika Wilaya hiyo yalikuwa asilimia 7 na kuonesha wasiwasi
kuwa uenda kiwango kikawa kinaongezeka kwa takwimu mpya zinazotarajia kutolewa
kwa siku za usoni.
Bw. Olesanare
amezitaja sababu zinazochangia ugonjwa huo kuwa ni baadhi ya wasichana na
wavulana kujiingiza katika mikesho ya majumba ya starehe, vigodoro pamoja na
wazazi na walezi kusahau wa wajibu wao wa malezi kwa vijana kwani wamewapa
uhuru wa kupitiliza lakini pia akiangazia mitandao ya kijamii kuwa nayo ni
kichocheo cha maambukizi hayo.
Askofu Mstaafu wa
Jimbo la Morogoro Baba Askofu Telesphor Richard Mkude amewataka wananchi kote
Nchini kuacha kumsingizia Mungu kuwa ndiye chanzo au sababu ya janga la UKIMWI
akiutaja kuwa ni upungufu wa hayo na ni upungufu wa siha ambao haustahili
kuwepo katika mwili wa mtu.
Aidha Askofu Mkude
amehitaka jamii kubadilika na
kujielimisha kwa lengo la kuondoa ujinga na kuhamua nakudhamilia kutenda daima
yaliyomema kwa Mungu na yaliyomema kwa wanadamu na tusisahau kuwa
tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na kwahiyo si wajinga wala masikini.
Kiongozi huyo wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro aliongeza kuwa sasa sio wakati wakulaumiana
kuwa nani mkosefu na nani mwema bali ni wakati wa kila mmoja wetu kujitazama
katika kioo na dhamira yake mbele ya Mungu na kujiuliza kama ni msafi na ameoga
katika neema ya mwenyezi Mungu au amejisafisha kadili ya mafundisho ya Mwenezi
Mungu na kujitathimini kama tuna tunayotenda ni mema mbele ya Mungu na mbele ya
watu wengine.
Aidha pamoja na maoni
hayo kutoka kanisa Katoliki Katibu wa Umoja wa Makanisa ya Kikristu Mkoani
Morogoro Mchungaji Canon Regnard Mdugi alitaja sababu ya vijana wengi kupata
maambukizi ni kuwa ni tamaa ya kuiga pamoja na
baadhi ya vijana wa kike kwenda katika majumba ya starehe kwa lengo
lakujipatia kipato.
Mchungaji Mdudi
alitoa wito kwa viongozi wenzake Mkoani Morogoro kushirikiana na kupambana na
maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI Mkoani Morogoro na kukemea vitendo viovu ili
kuwanusuru watu na janga hili kwa lengo la kulinda nguvu ya kanisa kuteketea na
janga hili la UKIMWI.
Wakati huo huo Shekhe
wa Mkoa wa Morogoro Shekhe Ahmad Khayrallah amewataka vijana wa Kiislam Nchini
kuwa na subira na kuacha vitendo vya zinaa kabla ya ndoa ili waweze kuachana na
tabia zozozte mbaya zitakazo watumbukiza katika machafu uku akiwaasa kusubiri
kuoa au kuolewa.
Shekhe Khayralla
ameutaja utandawazi kuwa umewafanya vijana kuachana na mila na desturi na kujikuta
wanasahau pia mafundisho ya dini lakini wengine bila kujua walijikuta wanaingia
katika lindi la madawa ya kulevya na matokeo yake kupata maambukizi ya virusi
vya UKIMWI.
Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku amesema kampeini ya Maambukizi ya Virusi vya
UKIMWI kwa Vijana imeendelea kwa Wilaya za Kilombero, Malinyi, na Ulanga na
imefanyika mashuleni na makundi mengine ya mitaani kwa kuwa maambukizi ya
UKIMWI kwa hivi karibuni yamekuwa yakipanda
No comments:
Post a Comment