Na Talib Ussi, Zanzibar
Mwanyekiti wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba wa chama cha ACT-Wazalendo Rashid Khalid Salim na wazake saba
wameachiwa kwa dhamana katika kituo cha Polisi Wilaya ya Micheweni.
Akizungumza na waandishi wa habari Habari Katibu wa katiba na sharia pamoja na haki za Binaadamu
wa Chama hicho Kombo mwinyi Shehe alisema kuwa watu wao tayari wameachiwa na
wametakiwa warudi tena kesho kituoni hapo kwa kukamilisha masharti waliokewa.
Shehe alisema kuwa
Jeshi la Polisi limewataka watu hao akiwemo Mwenyekiti wa ACT mkoa huo kupeleka mdhamini MMoja na laki Tano za maandishi.
“Alihamdulillah watu
tumewapata na sasa tunarudi nao nyumbani kuwapamoja na familia zao na kesho
tutarudi tena kukamilisha masharti waliyotuwekea” alieleza Shehe
Waliowekwa ndani ni
Rashind Khalid Salim (57), Abdi Khatib
Suleiman (42), Ali Rajab kombo (53) Abdallah Ali Said (48), Ali Said Faki (30) Hatib Saleh Juma (14) Pamoja na Said Shinei
Hamad.
Watu hao walikamatwa
tarehe 18 na 19 mwezi huu baada vibanda viwili vya makuti ambao vinamilikiwa na
wafuasi wa chama cha Mapinduzi katika Shehia ya Wingwi Mapofu Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Hali imekuja baada ya
kuaza kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuaza Pemba huku
wafuasi wa vyama vya Upinzani wakilalamika kunyimwa haki hiyo kutokana kukosa
Vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi ambacho kinawapa uwezo wa kufanya usajili huo
No comments:
Post a Comment