Kaimu Ofisa Mkuu wa
Biashara wa Tigo, David Umoh, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo Ujanja Ni, inayowawezesha wateja kuwa na uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko, William Mpinga. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA SULEIMAN MSUYA
KAMPUNI
ya Tigo imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Ujanja Ni’ ikiwa na lengo
la kuwapa wateja thamani ya pesa zao kila wanapotumia bidhaa zao.
Kampeni hii itawapa wateja uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi.
“Vifurushi
vyote vya sauti vinampa mteja uhuru wa kupiga simu mitandao yote kwa
bei ile ile. Huduma hii ni ya kwanza katika soko la simu na ni suluhisho
kwa wateja wa Tigo kwa sababu itaweza kubadili namna ambavyo watu
wanatumia huduma za mawasiliano hapa nchini,” ilisema taarifa.
Akizungumzia
fursa hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Ofisa Mkuu wa
Biashara wa Tigo, David Umoh huduma hizi zinampa mteja uhuru wa kupiga
simu kwenda mtandao wowote kwa gharama ileile.
Alisema
wateja wanaweza kununua kifurushi chochote cha dakika, intaneti au
vifurushi mchanganyiko na kufurahia faida zote muhimu kwa gharama nafuu
zaidi,”
Aidha, alisema vifurushi vyote vimeboreshwa kwa kuongezewa muda wa maongezi, SMS pamoja na intaneti.
Pia
alisema huduma hizi zinakuja pamoja na vifurushi vya wiki na mwezi ili
kumpa mteja uwezo wa kuwasiliana zaidi, kuperuzi na kupata thamani ya
pesa yake katika kila matumizi anayoyafanya.
Umoh
alisema kampeni hiyo inaendana na jitihada za Serikali za kuhakikisha
huduma za kupiga simu kwenda mitandao yote zinakuwa nafuu.
“Kama
kampuni ya kidigitali tunaamini kuwa huduma hii itasaidia kuongeza
uhuru wa mawasiliano na kuwaunganisha wateja wetu na wapendwa wao bila
mipaka kutoka Tigo kwenda mitandao mingine.
Tunaanzisha
huduma hii chini ya kampeni iitwayo ‘Ujanja ni’ ikiwa na maana kwamba
ujanja ni kutumia fursa hii ya kupiga simu kwenda mitandao yote ukiwa na
Tigo,” alisema Umoh
“Kwa
mara ya kwanza, zaidi ya wateja 12 milioni hawatakuwa na wasiwasi tena
pale wanapotaka kuwasiliana na watu waliopo kwenye mitandao mingine hapa
nchini. Hii inadhihirisha jitihada zetu za kuwa mtandao ambao unampa
mteja thamani zaidi kupitia huduma za kibunifu,” alisema Umoh.
No comments:
Post a Comment