NA TIGANYA VINCENT, TABORA
BARAZA la Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) limeishukuru Serikali kwa kuwapatia
shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kisasa
katika eneo la Isikizya.
Fedha hizo zitasaidia
katika ujenzi wa majengo ya fani mbalimbali iiwemo ushonaji, ufundi umeme ,
uhazili na komputya na uchomeleaji vyuma
(welding)
Kauli hiyo imetolewa leo
na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi wakati wa mkutano wa pili wa Baraza
la Madiwani wa kupitia taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Alisema kukamilika kwa
Chuo hicho cha VETA kutasaidia vijana ambao wamemaliza elimu ya Shule za Msingi
na Sekondari kusomea kozi mbalimbali ambazo zitawawezesha kujiajiri wenye kwa
ajili ya kuondokana na umaskini.
“Kwa kweli tunampongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutapatia
fedha hizo zitakazotuwezesha kujenga chuo cha kiasasa katika eneo la Isikizya…hii
inaonyesha kuwa anatupenda sana watu wa Uyui” alisema.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo alisema Hospitali ya Wilaya ya imeanza kufanya kazi kwa
kutoa huduma za matibabu ya wagonjwa wan je.
Alisema kuwa hatua hiyo
imefikia baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora la kumtaka Mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo kuanza na utoaji wa huduma za awali katika majengo ambayo
yamekamilika ili kuwapunguzia adha za wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma
za matibabu.
Alisema kwamba kuanza
utoaji wa huduma kwa Wagonjwa wa Nje(OPD) kumesaidia kupunguza usumbufu kwa
wananachi wa wilaya hiyo kwa kupata huduma za matibabu kuwa karibu na wananchi.
Wakati huo huo Ntahondi
alisema kuwa Halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi
wa majengo katika Sekondari saba ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi wa
Kidato cha kwanza.
Alisema sanjari na hilo
wanaomba Ofisi ya Kanda ya Udhibiti ubora kuwasaidia ili Shule ya Sekondari ya
Idete iweze kupokea wananfunzi wa Kidato cha Tano mwaka huu.
Ntahondi alisema
wanaendelea na wanaandalizi kwa ajili ya uanzishwaji kwa Kidato cha Tano kama
watakubaliwa ili Wilaya hiyo iweze na Shule za sekondari za Kidato cha tano na
sita mbili ikiwemo ya hivi sasa ya Ndono.
No comments:
Post a Comment