Sehemu ya makabidhiano ya baadhi ya misaada hiyo kati ya Jumuiya ya Wazazi na Shule ya Sekondari Kibeta.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Stella Buchwa akizungumza na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Yazid Issack, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibeta.
Wanafunzi Beatrice Christian wa Shule ya Sekondari Kibeta akitoa neno la shukrani baada ya kupokea misaada hiyo.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na Umoja wa Wanawake (UWT) Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera umetoa msaada wa kilo 500 za unga wa uji na kilo 100 za sukari katika Shule ya Sekondari Kibeta na Shule ya Msingi Kibeta ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli za elimu bure.
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM
chini ya Mwenyekiti wa UWT, Stella Buchwa, wametoa msaada huo wa kilo 500 za unga wa uji na sukari kilo 100 kiwa ni mwendelezo wa kusherehekea miaka 43 ya Chama hicho ili kuunga juhudi za Rais Magufuli katika masuala ya elimu bure na kuhamasisha wazazi na jamii kujenga utamaduni wa kujitolea ili watoto wao wapate huduma ya uji shuleni.
Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa UWT kata kibeta manispaa ya Bukoba, Stella Buchwa, amesema Jumuiya hiyo wametambua majukumu makubwa aliyonayo Rais Magufuli ya ujenzi wa taifa wakawiwa kuunga mkono juhudi kwa kutoa huduma ya uji kwa watoto wa shule.
Stella amesema wazazi na jamii wanapaswa kujenga tabia ya kujitoa kwani serikali ya awamu ya tano imefanya pakubwa.
Akipokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari kibeta iliyopo manispaa ya Bukoba Amos Kabunu amewaipongeza jumuiya hiyo pamoja na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Stella Deus ambaye amefadhili msaada huo na kudai kuwa suala la huduma ya uji shuleni hapo limekuwa changamoto kubwa kutokana na wazazi kutojitoa kikamilifu licha ya hamasa.
Kabunu amesema shule ya sekondari kibeta ina jumla ya wanafunzi 413 ambapo mwanzoni wanafunzi 200 walipata huduma hiyo na baadae zoezi kukwama hadi kufikia wanafunzi 32 tu waliokuwa wakipata huduma hiyo hadi sasa.
Salum Suleiman Omary na Bitrice Christian ni wanafunzi wa shule ya sekondari kibeta wametoa pongezi kwa Chama hicho na kuwa mwanzoni hawakupata huduma hiyo ambapo waliweza kukaa shuleni hapo asubuhi hadi jioni bila kuweka chochote tumboni jambo lililowafanya kutosoma masomo yao vizuri.
Wamedai kuwa kati ya wanafunzi 413 wanafunzi 32 ndio waliokuwa wakipata huduma hiyo.
Kwa upande wake katibu mwenezi CCM wilaya ya Bukoba mjini Yazid Issack amewahimiza wazazi kuwapenda watoto wao kwa kufuatilia mienendo ya watoto wao, kuwajali na kuwapenda na kuitaka jamii kujitolea katika makundi mbali mbali.

No comments:
Post a Comment