HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2020

HOSPITALI YA KAIRUKI YAFANYA UPIMAJI AFYA BILA MALIPO DAR

 
Baaadhi ya wagonjwa wakisubiri kupata huduma ya upimaji afya bila malipo katika Hospitali ya Kairiki jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
Fundi Mchundo wa Maabara wa Hospitali ya Kairuki, Joseph Mwakasagula (kulia), akimpima Selimundu, Abdulaziz Siwa, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki, iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya na magonjwa mbalimbali bila malipo jijini Dar es Salaam. 
   
Muuguzi wa Hospitli ya Kairuki, Anna Barampama, akimpima mgonjwa urefu kabla ya kupata matibabu.
 Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki, Grace Chiume, akimpima mgonjwa shinikizo la damu wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
 Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki, Nancy Mollel, akiwahudumia wagonjwa.
 Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki, Grace Chiume, akimpima mgonjwa shinikizo la damu wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
 Mgonjwa akipima uoni wa macho.
Muuguzi Idara ya Macho Hospitali ya Kairuki, Blandina Filbert, akipima kiwango cha uoni kwa kuwaonyesha herufi baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupima afya ya macho.
Muuguzi Idara ya Macho Hospitali ya Kairuki, Mzee Makolela, akipima kiwango cha uoni kwa kuwaonyesha herufi baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupima afya ya macho.
Baadhi ya wagonjwa waliofika Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya kupima afya bila malipo.
Baadhi ya wagonjwa waliofika Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya kupima afya ya macho wakisubiri kupata huduma hiyo ambayo ilitolewa bila malipo.
 Fundi Mchundo wa Maabara wa Hospitali ya Kairuki, Joseph Mwakasagula (kulia), akimpima Selimundu, Astrida Arnold, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki, iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya na magonjwa mbalimbali bila malipo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji wa afya na magonjwa bila malipo wakati wa maadhimisho ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki
Profesa Paschalls Rugarabamu akitoa mada katika mhadhara wakati wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki, iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya na magonjwa mbalimbali bila malipo jijini Dar es Salaam.  
 
Profesa Paschalls Rugarabamu akitoa mada katika mhadhara wakati wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki, iliyokwenda sambamba na upimaji wa afya na magonjwa mbalimbali bila malipo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
 Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
  Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki, wakiongozwa na mke wa marehemu Hubert Kairuki (mbele), Kokushubira Kairuki.
 Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.
Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, akifuatilia mda zilizokuwa zikitolewa katika  mhadhara wa Maadhimisho ya 21 ya Kumbukizi ya Prof. Hubert Kairuki.





Na Mwandishi Wetu

JOPO la madaktari zaidi ya sita wa Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam wameendesha zoezi la upimaji wa afya  bila malipo kwa wananchi wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwamo macho na saratani ya matiti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Onesmo Kaganda alisema wanatoa huduma hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya 21 ya kumbukizi ya Profesa Hubert Kairuki ambaye ndio mwanzilishi wa hospitali hiyo.

Alisema kwa siku mbili wananchi na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walipata fursa ya kupata vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti, seli mundu, macho, kuchangiaji damu, pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.

Dk. Kaganda alisema lengo la kutoa matibabu hayo ni kuhakikisha wanatoa mchango  wao katika jamii wakati wafanyaji kumbukizi hiyo ya Profesa Kairuki.

"Kambi hii ya siku mbili ilifanikisha utoaji wa huduma hizo bila malipo na tunashukuru wananchi wamejitokeza kwa wingi ambapo waliofika kupima Seli mundu (Sickle Cell) walikuwa 217, macho ni 344 na waliofanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti ni zaidi ya 70," alisema 

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa hospitali hiyo, Arafa Juba, alisema katika upimaji huo wale waliopima macho na kugundulika wanamatatizo katika upande wa kusoma, hospitali hiyo imewapatia miwani bure.

Aidha alisema katika kumbukizi hiyo pia kumefanyika mhadhara wa wazi uliyokuwa unahusu urithi wa Profesa Kairuki katika utoaji wa elimu juu ya Huduma za kitabibu.

Alisema anawashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi katika ufanyaji wa vipimo bila malipo na kuongeza kuwa hatua hiyo imewafanya waweze kutambua afya zao na kuanza kujikinga au kutumia dawa kama wamegundika na tatizo.

No comments:

Post a Comment

Pages