Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel
Chongolo akikagua mtambo uliokuwa ukikarabati Mto Salasala jana alipofanya
ziara ya kukagua mito ambayo imeathiriwa na watu waliokuwa wakichimba mchanga.
Watu waliokuwa wakifanya
shughuli ya kuchimba mchanga katika bonde la Mto Salasala wakipanda miti aina
ya miazi, Magugu kwa lengo la kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Nyumba zilizoko pembezoni mwa
mto Salasala zilizoathiriwa na bonde hilo.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi
ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha
athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo.
Vibali vilivyositishwa katika ni vile
vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi,
Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na
kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya
shughuli hizo.
Akizungumza mara baada ya
kufanya ziara katika Bonde la mto Salasala (Mto Tegeta) Mhe. Chongolo amesema kuwa amefikia uamuzi huo
baada ya wakandarasi waliopewa vibali hivyo
kuharibu mto huo na hivyo kuamuru kupandwa kwa Miti hiyo ambayo itasaidia
kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Amesema kuwa kinachofanyika hivi
sasa ni kurekebisha mito hiyo kwa kupanda miti, magugu pamoja na mianzi
inayoshika ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa undongo na hivyo kuweka mkakati wa kuratibu shughuli
za utoaji mchanga kufanyika katika maeneo hayo.
Mhe. Chongolo amesena kuwa katika
Halmashauri hiyo ameruhusu kibali hicho kutolewa katika bonde la Mpigi kwa maelekezo
ya kuhakikisha kuwa shughuli hizo zifanyike kwa ajili ya kusafisha mto ili
kuondosha adhari kwani mchanga ukijaa sana husababisha maji kusambaa nje.
“ Wakati tunafanya haya ni lazima tusitishe
shughuli zote zinazofanyika hapa, tulifanya tathimini ya kuangalia athari kwa
kuunda timu ambayo ilikamilisha majukumu yake na kuleta ripoti hiyo Disemba
mwaka jana, mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza mjadala na wale ambao walipewa
kandarasi ya kutoa mchanga kwenye mito hii” amesema Mhe. Chongolo
Nakuongeza kuwa “ baada ya
majadiliano hayo, tulikubaliana nao kupanda Miazi, Miti na Magugu, na watu ambao mnawaona hapa asilimia 90
niliagiza kila mwenye kibali cha bonde anayekuja aje na watu 10 kwa ajili ya
kushirikiana kupanda miti, na hii miti inayopandwa hapa sijanunua wameleta wao”
ameongeza Mhe. Chongolo.
Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa “ kwanza
mchanga usiondolewe kibiashara ,tutoe mchanga sehemu ambayo tunaona kuwa
kunaongezeko ambalo linaweza kusababisha athari, ili turuhusu maji yapite bila
kuleta madhara kwa wananchi waliopo pembezoni mwa mto na huyo anayetoa
ahakikishe anafanya marekebisho ikiwemo kupanda miti, magugu na mianzi.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo
amesema kuwa " Tunachangamoto ya watu kufanya shughuli za kibinadamu
kwenye maeneo ya maji, Serikali imeshaelekeza watu ambao wapo kwenye
maeneo haya wanatakiwa kuwa umbali wa mita 60 kwa 60 , lakini hatufuati hiyo Sheria
ya mazingira.
Wananchi mliopo katika maeneo haya,
niwasihi sana acheni kufanya shughuli hapa, leo tunapanda miti ili kunusuru
bonde hili lisiendelee kukua, mchanga utatolewa kwa kibali kwa ajili ya
kusafisha mto ila sio kuchimba mchanga kwa shughuli ya kibiashara ama nyingine,
" amesema Mhe. Chongolo.
No comments:
Post a Comment