Ndugu Wanahabari,
Napenda kupitia kwenu kuwajulisha kuwa hali ya ulinzi
na usalama nchini ni shwari kwani
uhalifu unaendelea kudhibitiwa.
Hata hivyo yapo matukio ambayo yamesababisha vifo kwa watanzania wenzetu
vilivyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na
tukio la waumini waliokuwa kwenye ibada ya maombi kule Mkoani Kilimanjaro
kukanyagana na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine takribani 16 kuumia
sehemu mbalimbali na wanaendelea na matibabu.
Ndugu wanahabari,
Tukio
lilitokea Mkoani Kilimanjaro ni tukio baya
kwani watanzania wenzetu walikwenda kwenye ibada lakini hawakutarajia
wangepoteza maisha.
Makongamano
na ibada za maombi zimefanywa mara nyingi kupitia viongozi wa madhehebu
mbalimbali na hakuna madhara yaliyotokea. Hata hivyo aliyeendesha ibada hiyo
kuanzia tarehe 30/01/2020 na tarehe 01/02/2020 ikiwa ndiyo ilikuwa hitimisho
amefanya ibada kama hizo maeneo mengine lakini hakuna madhara ambayo yamewahi
kutokea.
Ndugu wanahabari,
Kutokana na
hali hiyo ndiyo maana tukio hilo limechukuliwa hadi sasa kama taarifa ya vifo
na siyo mauaji. Jeshi la Polisi kama
ilivyoelezwa awali lilimkamata Boniface Mwamposa na wenzake walioandaa
kongamano hilo la ibada na kuchukua maelezo yao. Pia uchunguzi wa kina unaendelea kufanywa kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya dola na pale ambapo itabainika kwamba
kunakosa la jinai lilitendwa na kupelekea kutokea kwa vifo hivyo na majeruhi
hao hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika kwa mujibu wa sheria.
Aidha,
mapungufu watakayo yabaini katika uchunguzi huo yatasaidia kuweka mikakati
thabiti ili kuepusha madhara kama hayo kutokea tena katika mikusanyiko
mbalimbali.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na:
Davide A. Misime -
SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment