HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2020

Diwani Ajivunia Maendeleo Katika Kata Yake

Diwani wa Kata ya Somangila Wilaya Kigamboni, Chichi Masanja (CCM), akizungumza  na waandishi wa habari  mara baada ya  uzinduzi wa jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.


Na Asha Mwakyonde


DIWANI wa Kata ya Somangila Wilaya Kigamboni, Chichi Masanja (CCM), amesema tukio la uzinduzi wa jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya  Sara Msafiri ni hatua kubwa ya kimaendeleo katika Wilaya hiyo.

Fabruari 11, mwaka huu Rais John Magufuli amezindua jengo hilo pamoja na maabara kubwa tatu za kisaaa katika Wilaya hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani  ya Chama cha Mapinduzi ( CCM),

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika Februari 11, mwaka huu wilayani hapo, Masanja amesema Rais  Magufuli aliwapatia shilingi bil.15  ambazo zinetumika kujenga hospitali kubwa iliyopo katika kata yake ya Somangila.

Diwani huyo amesema wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliwaahidi wananchi kutilia mkazo kupigania suala la afya likiwamo la upatikanaji wa gari la wagonjwa katika manispaa ya Temeke kabla haijagawanywa kuwa Kigamboni.

"Namshukuru Rais Magufuli kwa maelekezo aliyoyatoa kuwa madiwani wa Wilaya ya Kigamboni tutembee vifua mbele na mimi natembea kifua mbele kwani moja ya ahadi zangu  kubwa kwa wananchi walionichagua imeshatekelezeka," amesema Masanja.

Masanja amesema amemuombea  Rais Magufuli Mungu amjaalie  aendelee kufanya kazi ya taifa na kwa upande wake ataandelea kuchapa kazi katika kata yake.

Aidha Masanja amekishukuru chama chake  CCM  ambacho kimempa ridhaa ya kusimamia  utekelezaji wa  Ilani.

No comments:

Post a Comment

Pages