Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao
chake cha Februari 13, 2020 ilipitia taarifa mbalimbali za mechi ya Ligi
Kuu Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili
(SDL) zinazoendelea hivi sasa.
LIGI KUU
Mechi
namba 197- Singida United FC 2 vs Mwadui FC 2. Mchezaji wa Mwadui
Hashim Yahya Mussa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu (TFF) kwa kosa la kuwaonyeshea kidole cha kati watazamaji kama
ishara ya matusi baada ya filimbi ya kumaliza mchezo ilipopigwa.kitendo
hicho kilifanyika katika mchezo uliofanyika February 8, 2020 katika
uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mechi
namba 200- Ruvu Shooting 0 FC vs Yanga SC 1-Timu ya Yanga SC imepewa
Onyo kali kwa kosa la kuwakilishwa na watu pungufu ya idadi inayotakiwa
katika kikao cha maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na kujaza jina
la Kocha wa walinda milango Peter Manyika kuwa amehudhuria kikao hicho
wakati hajahudhuria. Kitendo hicho kilifanyika katika maandalizi ya
mchezo uliofanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Uhuru Dar es
Salaam.
Onyo kali limetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 34 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi
namba 205- Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons FC. Tanzania Prisons FC
imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliokuwa
ufanyike Februari 11, 2020 baada ya timu ya Ruvu Shooting FC ambayo
ndiyo timu mwenyeji kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance)
uwanjani kama Kanuni ya 14 (2l) inavyosema na kusababisha mchezo
kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri kwa dakika 30 bila gari hiyo
kutokea.
LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi
namba 80 Gipco FC 1 vs Gwambina FC 2- Meneja wa timu ya Gipco Ayubu
Msonge amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Miguu Tanzania
(TFF) kwa kosa la kumpiga teke mwamuzi wa mchezo huo tajwa baada ya
mchezo kumalizika pindi waamuzi walipokuwa wanatoka uwanjani, kitendo
hicho kilifanyika February 08, 2020 katika uwanja wa Nyankumbu mkoani
Geita.
- Klabu ya Gipco
imetozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kutokana na timu hiyo
kushindwa kuhakikisha usalama kwenye mchezo uliofanyika February 08,
2020 katika uwanja wa Nyankumbu ikiwa ni jukumu lao kama timu mwenyeji,
hivyo kutokea vurugu zilizosababisha kupigwa kwa afisa wa Bodi ya Ligi
na waamuzi wa mchezo huo tajwa katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43 (1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Uthibiti wa Klabu.
Kamati
imeieleza timu ya Gipco FC kuwa endapo vitendo hivyo vitajirudia tena
katika mchezo mwingine watakaocheza, haitasita kuchukua maamuzi makubwa
zaidi ikiwemo kuwabadilishia uwanja wa nyumbani wa klabu yako (home
ground) na kupangiwa uwanja mwingine.
Mechi
namba 78- Transit Camp FC 4 vs Mawenzi FC 0-- Meneja wa timu ya Mawenzi
Fc Christopher Mapunda amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la
Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye
benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha za matusi katika mchezo huo
tajwa uliofanyika February 2, 2020 katika uwanja wa Uhuru jjini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment