Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, (kushoto) akioneshwa kitu
juu ya ghorofa na Meneja majengo na Mbunifu majengo kutoka Wakala wa
majengo (TBA) Benard Mayemba, kulia baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa
majengo ya nyumba za makazi ya wakaazi wa magomeni Kota Dar es Salaam,
baada ya kufanya ziara hiyo.
NA FARAJA EZRA
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo, amewataka wananchi wa magomeni
kota kulipa kodi ya majengo kwa wakati ili kuepuka ulimbikizaji wa
madeni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini humo wakati akizindua kampeni ya
Uhamasishaji wa Ulipaji kodi pamoja na kukagua majengo hayo ambapo
alisema kila mwananchi atakayetakiwa kuishi kwenye majengo hayo
atatakiwa kulipa kodi mapema hadi juni 30 mwaka huu.
Aidha
Chongolo alisema wananchi wengi wamekuwa wakilimbikiza kodi mwishowe
hushindwa kulipa kutokana na ukubwa wa gharama hivyo ili kuepukana na
adha hiyo watatakiwa kulipa mapema.
"Tuache
tabia ya kusubiri dakika za mwisho Kama ilivoyokea kwenye usajili wa
laini za simu kwa alama za vidole, nawasihi wananchi wangu muanze kulipa
sasa," alisema Chongolo.
Alisema
kwa nyumba ya kawaida lililopo kwenye kiwanja kimoja mwananchi
atatozwa shilingi 10,000/=lakini kwakila sakafu nyumba ya ghorofa moja
ya ghorofa atatakiwa kulipa 50,000/=.
"Kampeni
hii ya uhamasishaji imeanza hii leo na kilele chake ni Juni 30 mwaka
huu na kwamba ifikapo mwezi huo makusanyo yote yawe yamekamilika"
alisema Chongolo.
Naye
Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Makazi wa Magomeni Korter Act. Benard
Mayemba, alisema Ujenzi huo unasimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) ambapo imejengwa jumla majengo matano yenye ghorofa nane huku
ikiwa na uwezo wa kuhifadhi wakazi zaidi ya 644.
Mayemba
alieleza kuwa Ujenzi huo umefikia hatua nzuri ambayo kwa makadirio
imefikia asilimia 69 na wanatarajia kukamilisha Ujenzi huo Aprili mwaka
huu.
" Wakazi wa Magomeni
wanasubiri kwa hamu ukamilishwaji wa Mradi huu ili wapate Makazi Bora
na ya kudumu, hivyo serikali kwa kushirikiana na sisi tunafanya kila
jitihada kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya Makazi" alisema
Act. Mayemba.
Mbali na
hiyo Mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa wakazi wa magomeni kwanza
imetoa fursa mbalimbali za ajira kwa vijana lakini pia mamantilie.
No comments:
Post a Comment