Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro
akimkaribisha Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za ukanda wa
Kusini mwa Afrika (SARPCCO) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Zimbabwe Kamishna
Jenerali Matanga leo Makao Makuu ya
Polisi jijini Dar es Salaam. (Picha na Hassan Mndeme - Jeshi la Polisi).
Na
Tamimu Adam – Jeshi la Polisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Tanzania inanufaika kiulinzi
na usalama kutokana na kuwa mjumbe wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za
ukanda wa Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
IGP Sirro alisema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari mara baada ya
kikao na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Polisi
Zimbabwe, TG Matanga ambaye yupo nchini kwa ziara maalum.
Aliongeza kuwa kutokana na Tanzania
kuwa mwanachama wa shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi zilizopo kusini mwa
Afrika Tanzania, imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuzuia na kudhibiti makosa yanayovuka mipaka yakiwemo makosa ya usafirishaji
haramu wa binadamu, wizi wa magari pamoja na dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Zimbabwe, Kamishna Jenerali TG
Matanga, alisema yupo hapa nchini kwa ziara maalum ya kufanya tathmini ya
utekelezaji wa maazimio ya INTERPOL pamoja na maazimio ya SARPCCO.
Kamishna Matnga alisema operesheni za
pamoja zinazofanyika kwa kushirikiana baina ya nchi mbili, operesheni za kikanda pamoja na kimataifa kama operesheni Usalama zimeonesha mafanikio makubwa baina ya nchi wanachama
katika uhalifu wa ndani na ule unaovuka mipaka , hivyo ameitaka Tanzania
kuendelea kuwa mstali wa mbele katika operesheni mbalimbali zinazoratibiwa na
shirikisho hilo.
Aliongeza kuwa, ili kuimarisha shirikisho hilo ni muhimu kuwekea
msisitizo eneo la mafunzo ya pamoja ili kupambana na wahalifu na uhalifu unaovuka mipaka.
No comments:
Post a Comment