HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2020

KYERWA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA TUNU KUBWA YA UWEPO WA SEKTA YA UTALII, YAJIPANGA KUKUZA SEKTA HIYO

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Rashid Mwaimu, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.



Na Lydia Lugakila, Kagera

Kauli hiyo imebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Rashid Mwaimu katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

 Rashid Mwaimu akizungumzia vipaumbele mbali mbali vya halmashauri hiyo ametaja mambo mengi na makubwa yaliyofanywa na Rais wa jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo Afya , elimu, maji, na nyinginezo na kuwa wilaya ya Kyerwa ni wilaya ambayo inatarajia kuwa na utajiri mkubwa sana katika nyanja ya utalii kutokana na kuwa na mbuga mbili tofauti na  wilaya nyinginezo hapa nchini.

Akitoa pongezi kwa Rais Magufuli mkuu wa wilaya hiyo amesema wananchi wanapaswa kuchangamkia fulsa hiyo yenye utajiri kwani tayari mtetezi wao ametoa zawadi kubwa kwa wilaya hiyo hivyo juhudi binafsi zinahitajika ili kumuenzi Rais Magufuli kwa tunu hiyo ya utalii kwa wana Kyerwa.

" Hakika huu ni utajiri kwa wananchi wa Kagera hakuna biashara yenye fedha kama hii utalii tuupokee tufanye biashara tuongeze kipato "alisema Mwaimu.

Amesema ni wakati sasa kwa wananchi wilayani humo kutengeneza fedha kwa uhakika kwa kujenga maduka ya kiutamaduni, vyakula vya asili, mahoteli ya kuvutia, pamoja na  kuboresha huduma ya vyakula ili kuongeza mvuto kwa watalii watakaoingia hapa nchini.

Amesema wananchi wanapaswa kushirikiana na shirika la hifadhi za Taifa- TANAPA ili kuhakikisha utalii unaimalishwa.

Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa katika kumuenzi Rais Magufuli wananchi wahakikishe wanatunza hifadhi hizo ili zibaki katika ubora.

Amesema anatambua mchango mkubwa kwa TANAPA kwani wanatoa karibia 70% ya mradi huo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano huo.

Kutokana na hatua hiyo mkuu wa wilaya hiyo amemwagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Shedrack Mhagama kuhakikisha anasaidia utoaji mafunzo kwa wanawake wajasiliamali(mama  Lishe) ili wawe na ujuzi Zaidi katika kuandaa vyakula vizuri na vyenye  kuvutia watalii.

Hata hivyo ametoa onyo kwa wale wote wanajihusisha na kuchoma moto misitu na kuharibu vyanzo vya maji kuacha Mara moja tabia hiyo na kuahidi kuwasaka na kuwashughulikia ki sheria

No comments:

Post a Comment

Pages