HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2020

TANZANIA NA KUWAIT KUIMARISHA USHIRIKIANO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wilbert Ibuge (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kusheherekea Uhuru nchi ya Kuwait. Kulia ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mubarak Mohammad.


Na Asha Mwakyonde

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wilbert Ibuge, amesema urafiki wa Tanzania na  nchi ya Kuwait ni wa enzi wanashirikiana katika maeneo mbalimbali.

Haya aliyasema jijini Dar es Salaam  Februari 20, mwaka huu kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi wakati wa kusheherekea siku ya kumbukizi  ya Uhuru wa nchi ya Kuwait alisema  siku hiyo ni kubwa kwa nchi hiyo.

Katibu Ibuge amesema kuwa siku hiyo pia ni siku ya  mwaka wa 14  ambapo Mkuu wa Kuwait Mtawala  Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al- Sabah anasheherekea kulingaba na utawala wake.

Ibuge amesema maaeneo mengi  wanayoshirikiana na nchi ya Kuwait ikiwamo maji na afya ambapo tayari imeshasaidia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali ya Benjamin Mkapa, Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili ( MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (/JKCI).

" Watanzania tumekuja kuenzi ushirikiano huu. Nawapongeza Kuwait wanaendelea kukua katika maeneo yote afya na uwekezaji  wa maeneo mengine kama vile Maji," alisema.

Ameongeza kuwa wanapokea wawekezaji kutoka nchi ya Kuwait  na kwamba mahusiano yao yataendelea kukua.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mubarak Mohammad amesema kuwa anafura kuunga na Watanzania kusheherekea miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo.

Amesema ushirikiano wa nchi mbili kati ya Tanzania na Kuwait umeendelea kuweka alama kwa baadhi ya sekta na kwamba hadi kufikia hapa Tanzania imepata miradi ya maendeleo  14 ambayo imegharimu zaidi ya dola milioni 248.

No comments:

Post a Comment

Pages