HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2020

Maandalizi mbio za ‘Relay’ Taifa yaiva

MAANDALIZI kulekea mashindano ya Kupokezana Vijiti ‘Relay’ Taifa yanayotarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari 22 mwaka huu, yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Mashindano hayo yatashirikisha mbio za mita 100X4 na 400X4 yakishirikisha wanariadha kutoka mikoa tisa waliofikia viwango maalumu vilivyowekwa na Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya RT, Robert Kalyahe, maandalizi yamekamilika kwa asilimia 95 na tayari mikoa imetuma majina ya washiriki wao, ambao wamepatikana baada yam bio za majaribio ‘trials’ walizofanya huko.

“Tunaamini viongozi wa mikoa wamezingatia viwango tulivyotoa na hakuna udanganyifu, hivyo tunategemea ushindani utakuwa mkubwa sana na tutapata timu nzuri,” alisema Mjumbe huyo wa Kamati ya Ufundi wa RT.

Aliwaomba wadau na wapenzi wa michezo, kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kwani kiingilio ni bure.

Wanariadha watakaoshiriki na wanakotoka kwenye mabano ni Winfrida Makenji, Emmy Hosea, Ali Khamis Gulam, Hassan Khamis Ali, Naima Ali Musa, Abdallah Issa Khamis , Mohammed Ali Mshamba na Simai Kombo Haji (Zanzibar).

Wengine ni Binamunzi Katunzi, Ismail Tossil na Diana Matemu (Dodoma), Daniel Mussa, Elisha Machungwa, Japhet Kitungu (Mara), Boniface Inalo, Benjamin Michael, Jumanne Chacha, Andrea Robi (Arusha), Elias Sylvester, Selemani Sabin a Jeremiah Baruti (Dar es Salam).

Pia wamo Ramadhan Omary, Fahadi Juma, Petro Joseph (Singida), Jacob Lugaila (Mwanza), Bora Hassan (Tabora), Matondo Magembe, Rose Lucas, Thereza Benard, Rahel Nilla (Simiyu), Benedictor Mathias, Regina Mpigachai na Amos Charles (Pwani).

No comments:

Post a Comment

Pages