HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2020

UTATA WAGUBIKA KIFO CHA KATIBU WA ZAMANI UVCCM MULEBA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi.


NA LYDIA LUGAKILA, KAGERA

ALIYEKUWA Katibu  wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Katoke, wilayani Muleba mkoani Kagera, Jaspa Jasson, 41, amefariki dunia katika mazingira tatanishi, yanayoibua maswali kama amenyongwa au amejinyonga.


Akithibitisha kutokea kwa kifo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa kifo hicho kimetokea Februari 17, 2020 majira ya saa 1:30 asubuhi katika eneo la Kakindo, Kitongoji cha Kishenge, Kijiji cha Bisore, wilayani Muleba mkoani humo.

Kutokana na kifo hicho  Kamanda Malimi amedai kuwa, uchunguzi wa chanzo cha kifo unaendelea na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa huenda Jasson amenyongwa au amejinyonga.

No comments:

Post a Comment

Pages