HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2020

SEKONDARI YA RUKINDO YAPONGEZWA

 Mbunge wa Muleba Kusini mkoani Kagera Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na wananchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilayani Muleba, Athuman Kahara, akizungumza na wananchi.



Na Lydia Lugakila, Kagera

Mbunge wa Muleba Kusini mkoani Kagera, Prof. Anna Tibaijuka, kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo wamepongeza juhudi za Mwalimu Catherine ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Rukindo kwa kusimamia vema suala la mimba kwa wanafunzi huku kiwango hicho kikitajwa kushuka kutoka mimba 26 mwaka 2019 hadi mimba 4 kwa mwaka huu 2020.

Prof. Anna Tibaijuka ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara na hospitali ya Buganguzi iliyopo wilayani humo sambamba na kuongea na wananchi.

Prof Tibaijuka akiwa ameambatana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM  Athumani Kahara wametembelea miradi hiyo ya maendeleo  ambapo Mbunge huyo ameongea na wananchi na kumpongeza Mwalimu Catherine ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari ya Rukindo kwa juhudi za kusimamia suala la mimba shuleni hapo ambalo lilisababisha kuwepo kwa mimba 26 mwaka 2019 na mwaka huu wa 2020 kupungua hadi kufikia mimba 4.

Mbunge huyo amesema hali hiyo yenye mafanikio imekuja kutokana na Mwalimu huyo kusimamia vema suala hilo ambalo alihakikisha wanafunzi hao wanapimwa kila baada ya miezi mitatu.

Prof Tibaijuka amesema kutokana na jitihada hizo za mwalimu hataki kuona au kusikia wazazi wa wanafunzi hao wanamsumbua bali wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa.

Prof. huyo pia ametoa shukrani kwa Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani humo Athuman Kahara kwa kusimamia shughuli za maendeleo.

Aidha amempongeza Rais John Magufuli kwa namna ambavyo ametekeleza na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wake.

Katika hatua nyingine amewahimiza vijana kuomba mikopo na kufanya kazi kuliko kutegemea shughuli moja ya kuendesha piki piki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Athuman Kahara, amekemea wenyeviti wa vijiji wanaojihusisha na uuzaji wa ardhi ya kijiji kuacha Mara moja suala hilo vinginevyo wataondolewa katika nafasi zao.

No comments:

Post a Comment

Pages