Mkuu wa Wilaya ya Mahenge, Ngollo Malenya, akipeana mkono wa pongezi na John De Vries ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni Mahenge Resources inayoshughulika na uchimbaji madini ya Kinywe, katikati ni Waziri wa Madini
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya, akionyesha funguo za majengo yaliyojengwa Mahenge Resources.
Viongozi wa Kampuni ya Mahenge Resources.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akiwa na John De Vries ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Black Rock Mining.
Waziri wa Madini Dotto Biteko (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya (wa pili kulia) wakizindua majengo matatu ya serikali za kijiji yaliyojengwa na Kampuni ya Mahenge Resources.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Uchimbaji madini ya Kinywe, Mahenge Resources,
imekabidhi majengo matatu yatakayotumiwa na vijiji vya Kisewe,Mdindo na
Nawenga.
Majengo hayo ya kisasa yatakuwa ofisi za serikali ya vijiji
hivyo.
Akizungumza Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mtendaji Mkuu wa kampuni
ya Mahenge Resources, John De Vries, alisema lengo la kampuni yao ni
kuhakikisha wanaboresha maisha ya watu wengine hasa katika maeneo ambayo uchimbaji
wa madini unafanyika.
Vries alisema kurejesha kwa jamii ni wajibu na deni kwao.
“Kuwapa funguo wananchi ni deni la Mahenge Resources ili kuleta
uthamini, haki na namna ya usawia kwa watu wote,”alisema.
Alisema kwasasa kampuni hiyo inatarajia kufanya tathimini ili
kulipa fidia wananchi kabla uchimbaji wa madini haujaanza rasmi.
“Lazima tuhakikishe tunalipa fidia wananchi kabla hatujaanza
ujenzi wa mgodi na kuchimba, awali tulishapeleka sampuli za madini ya kinywe
kwenye maabara za kimataifa na kutoa majibu bora,”alisema.
Waziri wa Madini, Dotto Biteko, alisema kupitia mgodi huo wananchi
watapata ajira za kitaalam na zisizokuwa za kitaalam kupitia kufanya biashara
na hivyo kupata fursa ya kuuza vitu mbalimbali katika mgodi huo.
“Hii inamaanisha sehemu kubwa ya fedha zitokanazo na mgodi
zitabaki hapa hapa Tanzania, naitazama Mahenge Resources kama mradi
utakaofungua njia kwa awamu hii mpya ya migodi mikubwa na ya kati nchini ambayo
itafunguliwa,”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya, wanashirikiana na
Mahenge Resources kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Alisema kampuni hiyo inashiri katika kuchangia elimu, kulea
watoto yatima, kujenga madarasa na ofisi za vijiji.
No comments:
Post a Comment