NA MWANDISHI WETU
MBUNGE
wa Kilwa Kusini, Said Bungara (CUF), maarufu Bwege amesema Watanzania
wataendelea kupeleka malalamiko katika nchi zenye nguvu na taasisi
mbalimbali duniani kutokana na Serikali kutotaka kuwasikiliza
wanapowafikishia malalamiko yao.
Aidha,
Bwege amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuachana na
utaratibu wa kukubali kila jambo linalosemwa na Serikali kwani sio kazi
iliyowapeleka bungeni.
Mbunge
huyo alisema hayo wakati akichangia mjadala bungeni ambapo aliweka wazi
kuwa hawatasita kwenda kulalamika hadi hapo Serikali itakapoanza
kuwasilikiza na kutatua changamoto zao.
“Leo
tunaongea, tunasema hapa Serikali inajifanya masikio hayasikii ndio
maana watu wanaenda kusema Marekani huko, nyie hamsikii, mtu akipambana
anapambana kwa njia yoyote ndani na nje ya nchi.
Akienda
mtu nje ya nchi ooh msalitim, msaliti gani wakati nyie hamsikii, mimi
niliwambia waislam wamepigwa risasi wameuliwa Serikali ipo kimiyaaaa,
msaliti nani, tukiwambia hamsikii mnaangalia nani kasema hamuangalii
nini kasema,” anasema.
Kutokana
na uchangiaji huo Spika Job Ndugai aliingilia kati na kumshauri Bwege
achangie vizuri kutokana na suti ambayo aliiva siku hiyo.
“Mheshimiwa
Bungara nitakumbukumbusha neno moja kwa suti uliyovaa leo bluu bahari
inataka upige taratibu taratibu leo upo vizuri,” alisema.
Baada
ya Spika kuchombeza Mbunge huyo machachari aliendelea kuchangia kwa
kuwalaumu wabunge hawa wa CCM kwa kile alichodai kuwa hawasimamia
Serikali bali wanasifia jukumu ambalo sio lao.
Bwege
aliwaambia wabunge watambue kuwa wao ni wabunge wa Bunge la Tanzania na
sio CCM au CUF hivyo waachane na utaratibu wa kila kitu Serikali
ikisema liwe baya ndio zuri ndio ‘why’.
“Wabunge
sasa hivi tumekuwa kama mbumbumbu, umeshiba eeeh, una njaa eeh
‘why’unachosimamia hukijui kazi yao kusimamia Serikali,” alisema Bwege.
Katika
hali ambayo ilionesha kueleweka Spika Ndugai aliingilia tena kwa
kuwahoji wabunge wa CC. “Jamani wabunge wote wa CCM mmepigwa ganzi
hakuna hata raarifa alimalizia Spika Ndugai.
Pamoja
na madongo hayo Bwege aliisifia Serikali katika usambazaji wa umeme
vijiji na kuwataka waendelee kusambaza huduma katika sekta zote.
“Kusema
ukweli kwa umeme, Alhamdulilah mmetufikisha vizuri na kama mtaendelea
hivi kuhusu umeme mkaongeza kasi kwenye maji, mkawalipa wakandarasi,
mkalipa wakulima wa korosho, mkawa kesi za kubambikia hakuna.
Mkaongeza
mishahara kwa wafanyakazi, maandamano yawepo CCM yashinda na masheikh
waliokaa ndani miaka nane wakaachiwa CCM dole,” alisema.
Alisema
iwapo sifa itakuwa sifa ni umeme, masheikh hawatoki, mishahara
haiongezi, wakulima hawalipwi na mengine mengi CCM wahesabu kuumia 2020.
Aidha, aliwapa angalizo wasifurahie kuwa pekee yao bungeni kwa kiwi watafarakana na hawatafanya jambo loote la maana.
Alitolea mfano Zanzibar ambapo CCM wapo peke yao na hakuna jambo la ajabu ambalo limefanyika.
No comments:
Post a Comment