Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) - Mhe. Selemani Jafo akisalimiana na Mkuu wa Idara ya
Huduma za Serikali wa Benki ya NMB - Vicky Bishubo walipokutana katika
mkutano wa utoaji taarifa ya mafanikio ya TAMISEMI
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB imesema itahakikisha inaendelea na kuunga mkono juhudi za
maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano ili kuifikia malengo
yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)- Mhe. Selemani Jafo
akimkabidhi taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya wizara hiyo Mkuu wa
Idara ya Huduma za Serikali wa NMB - Vicky Bishubo mara baada ya
kuwasilishwa mwisho wa wiki, Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri
Wizara hiyo Mhe. Mwita Waitara.
.
Na Mwandishi Wetu
Kauli hiyo ilitolewa Mkuu
wa idara ya huduma za Serikali wa benki ya NMB, Vicky Bishubo wakati
alipokuwa akiwasilisha taarifa ya benki hiyo kwenye mkutano wa utoaji
taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) uliofanyika Jijini Dodoma.
“Benki
ya NMB ni mali ya wananchi na Serikali hivyo tunafurahi tunapoona kila
upande unaendelea kuiunga mkono katika mafanikio yaliyopatikana hivyo
tunawaomba mwendelee kutuunga mkono kwa kufungua akaunti na kuweka
fedha kwetu”alisema.
Bishubo
alisema Benki ya NMB itahakikisha inaendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali ili kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wake katika maeneo
mbalimbali nchini.
Alisema
benki hiyo inaendelea kufungua matawi na kuweka mashine za ATM katika
maneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za
kibenki karibu na maaneo yao.
Alibainisha
kuwa uwepo wa benki hiyo katika kila Wilaya hapa nchini imesaidia pia
kurahisisha maendeleo ya wananchi kwa kupata huduma za kifedha karibu
kwenye maeneo yao. Aliongeza
pia benki hiyo imeweka mawakala wengi hapa nchini kwa lengo la
kuwasogezea wananchi huduma za kifedha katika maeneo yao.
Aidha
alisema benki hiyo imekuwa ni sehemu ya mafanikio ya Ofisi ya Tamisemi
kutokana na kufanyakazi kwa karibu na Halmashauri zote hapa Nchini.
Kwa
upande Waziri Selemani Jafo alitaja baadhi ya mafanikio ya Ofisi hiyo
kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya 97 zimejengwa na vingine kukarabatiwa
na Serikali katika kipindi hicho cha miaka minne ya mafanikio
Jafo
alitaja mafanikio mengine kwenye sekta ya elimu kuwa ni ongezeko la
ufaulu wa wanafunzi, ujenzi wa vyumba vya madarasa na ukarabati wa
majengo ya shule kongwe hapa nchini.
Hata
hivyo aliwashukuru benki ya nmb kwa kuendelea kushirikiana na Serikali
kwa kutoa misaada mbalimbali kwenye sekta ya afya na elimu hapa nchini.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment