Ndugu waandishi wa Habari,
Nimekuwa nikipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza maendeleo ya uchunguzi wa tukio la watanzania wenzetu 20 waliopoteza maisha huko Mkoani Kilimanjaro baada ya kukanyagana kwenye hitimisho la kongamano la ibada ya maombi tarehe 01.02.2020 na hatma ya waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la polisi.

Kama ilivyokwisha kuelezwa na viongozi mbalimbali na kwenye taarifa yangu kwenu ya tarehe 03.02.2020 hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ni kwamba baada ya tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro (IGP) alituma timu ya maofisa wakiwepo wataalamu wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwenda kuungana na timu ya wataalamu kule Kilimanjaro katika uchunguzi.
Ndugu waandishi wa habari,
Katika uchunguzi huo walikamatwa watu nane (8) akiwepo
Bonifase Mwamposa na kuhojiwa kwa kina na baada ya
kujiridhisha na yale yaliyokuwa yanahitajika kutoka kwao
wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria ili waendelee kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.

Uchunguzi bado unaendelea na baada ya kukamailika
yatakayobainika yatatolewa na mamlaka husika na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu.

Hivyo kila mmoja anatakiwa awe na subira na uchunguzi unaofanywa na wataalam utakapokamilika mtajulishwa.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na:
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment