HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 13, 2020

Serikali ya Muungano, SMZ kuendeleza ushirikiano

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo katika kikao kazi cha mashirikiano kwenye Sekta ya Ujenzi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika kisiwani Pemba.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mustafa Aboud Jumbe, akizungumza jambo wakati akifunga kikao kazi cha mashirikiano kwenye Sekta ya Ujenzi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika kisiwani Pemba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nyumba na Nishati kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Ali Khalil Mirza, akishauri jambo wakati wa kikao kazi cha mashirikiano kwenye Sekta ya Ujenzi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika kisiwani Pemba.
Wajumba kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiwa katika kikao kazi cha mashirikiano kwenye Sekta ya Ujenzi baina ya Serikali hizo, kilichofanyika kisiwani Pemba.




Na Mwandishi Wetu
 

SERIKALI ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zimesema zitaendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo miundombinu na usafirishaji ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Msanifu Majengo na Majenzi Elius Mwakalinga, wakati akifungua kikao kazi cha mashirikiano kwenye sekta ya ujenzi, baina ya Serikali hizo kilichofanyika Kisiwani Pemba Zanzibar
Mwakalinga, alisema kuwa kupitia taarifa za utekelezaji ambazo  wakurugenzi wa taasisi wameagizwa kuziwasilisha kwao, zitawsaidia wao kama watendaji wakuu kujua namna gani ya kutatua chagamoto hizo kwa pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea.
“Hatukuongea kipropaganda, tumeongea kitaalaam namna ya kuboresha miundombinu na usafirishaji na tumepata maoni kutoka kwa wajumbe namna ya kuondosha changamoto katika masuala haya kati ya Serikali hizi”, alisema Katibu Mwakalinga.
Aidha, Mwakalinga, alifafanua kuwa mkutano huo ni endelevu kwani nia na madhumuni yake ni kuhakikisha wanajadili changamoto na kupata maoni ya wataalam kwa pamoja ambayo yatasaidia katika kuboresha na kufanikisha maendeleo katika sekta ya ujenzi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe, alisema lengo la kikao hicho ni kubadilishana uzoefu.
Alisema kikao hicho kimeazimia kwa kuwaagiza wakuu wa taasisi ambao ni wajumbe katika kikao hicho kuandaa taarifa zao za utekelezaji na kuonesha changamoto zao ili kwa pamoja ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Ali Khalil Mirza, alisema kuwa kupitia vikao hivyo wataalamu kutoka pande hizo mbili watashauriana na kubadilishana uzoefu ambao utasaidia kuboresha utendaji kazi katika maeneo ya kazi.
Mkurugenzi kutoka Kitengo cha Usalama na Mazingira, Mhandisi Julius Chambo, alisema Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar (SMZ),  inashauriwa kuanzisha mizani katika barabara zao ili kuzilinda na ziweze kudumu kwa muda mrefu pamoja na kuweka mifumo ya kisasa ambayo itasaidia kupunguza mianya ya rushwa.

No comments:

Post a Comment

Pages