Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(kulia),akiangalia moja ya darasa linalotumika kufundishia wanafunzi
katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni
lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma
zinazotolewa na Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameutaka uongozi wa Shule ya Polisi
Tanzania kuwafundisha ueledi wapelelezi ili kuweza kupunguza msongamano wa
mahabusu na kesi ambazo zinasababishwa na upelelezi usio na kiwango.
Masauni ameyasema hayo
mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya kutembelea Shule ya Polisi Tanzania lengo
ikiwa kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma za
Jeshi la Polisi.
“Mheshimiwa Rais Dkt.
John Magufuli alipokua akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria aligusia
suala la wapelelezi kuwa chanzo cha mlundikano wa mahabusu katika magereza yetu
na mimi hii leo nimetoka gereza la Arusha nimeongea na wafungwa na mahabusu nao
wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kupindishwa na mbaya zaidi wengine
wamehukumiwa vifungo kwa ajili ya upelelezi usio makini.Ni tatizo kubwa
haiwezekani Rais huyu alalamike kila siku sasa maagizo ya serikali kwa chuo
hiki jitahidini kupika vizuri wapelelezi wenu vizuri,tumpumzishe Rais wetu ana
mambo mengi,timizeni tu wajibu wenu”amesema Masauni
Akizungumza katika
ziara hiyo Kaimu Kamandanti Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar amesema
wamechukua maelekezo ya serikali na wanaahidi kuyafanyia kazi ili yaweze kuleta
tija huku akitaja idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo wakisomea fani mbalimbali.
“Shule yetu kwa sasa
ina wanafunzi 856 kati yao wanaume 725 na wanawake ni 131 ambao wako katika
mafunzo mbalimbali na wote wanaendelea vizuri na masomo” amesema Kamishna
Msaidizi Omar
Katika ziara hiyo Naibu
Waziri Masauni alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo
ikiwemo sehemu za kulala,madarasa,uwanja wa paredi,vyumba vya komputa na
ukarabati bwalo la chakula.
No comments:
Post a Comment