HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2020

Sita wanukia kuunda timu ya Taifa mbio za kupokezana vijiti 'Relay'

Mshindi mita 100 wanawake, Winifrida Makenji kutoka Zanzibar, akimaliza mbio hizo wakati wa mashindano ya kusaka viwango vya kuunda timu ya Taifa ya Mbio za Kupokezana Vijiti ‘Relay’ yaliyoandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mshindi wa kwanza mita 400 waume, Mohammed Ally kutoka Zanzibar, akimaliza mbio wakati wa mashindano yalioandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania RT yaliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpik nchini Japan.
 
 

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya mwisho kuunda timu ya Taifa ya Mbio za Kupokezana Vijiti ‘Relays’ yamefanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana huku ikishuhudiwa wanaume wakifanya vema kuliko wanawake katika kufikia viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Mashindano hayo yaliyokuwa ya kuhitimisha ‘trials’ mbalimbali zilizokwishatangulia mikoa mbalimbali, yalishirikisha wachezaji waliofikia viwango vilivyowekwa na Kamati ya Ufundi ya RT kutoka mikoa 11 ya Tanzania Bara na Visiwani, huku ikishuhudiwa ushindani mkali ukiwa kwa upande wa wanaume kuliko wanawake.

Lengo la mashindano hayo, ilikuwa kupata wachezaji wa kuunda timu za Relay mita 100X4 na 400X4.

Katika mbio za Mita 100 wanaume  kulikuwa na ‘heats’ tatu ambako ya kwanza Joseph Williamalishinda akitumia sekunde 11.66 akifuatiwa na Amos Safari    11.96, Lazaro Charles 11.97 wa tatu huku nafasi ya nne ikienda kwa Samwel Msila 12.13 na wa tano Hussein Hamisi        12.55 wote kutoka Dar es Salaam.

‘Heat’ ya pili, Ali Hamis Gulam alishinda akitumia sekunde 10.40 akifuatiwa na Hassan Hamis 10.90 wote kutoka Zanzibar na watatu akaibuka Binamungu Katunzi wa   Dodoma sekunde        10.91.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Jeremiah Baruti wa Dar es Salaam    sekunde 11.70 wa tano Boaz Benesta wa Simiyu   12.08, wa sita Jacob Lugaila kutoka Mwanza        12.22 huku wa saba ni Fande Juma     wa Singida   sekunde 12.38.

Katika heat ya tatu wanaume, Elias Sylvesterwa Dar es Salaam alishinda akitumia sekunde 10.66 akifuatiwa na Abdallah Issa kutoka    Zanzibar 10.72 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Ismail Husseinwa  Dodoma       10.91.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Selemani Kengwa wa Dar es Salaam    11.10 wa tano   Daniel Mussa kutoka Mara      11.53 huku nafasi ya sita ni Japhet Kitugo wa    Mara     12.05 na wa saba ni Ramachani Omari    kutoka Singida sekunde        12.21.

Mita 400 Wasichana kukikuwa na ‘heat moja, ambapo ilishuhudiwa Jane Maiga wa Dar es salaamu akishinda baada ya kutumia sekunde 59.37 akifuatiwa na Theresia Benard Simiyu        01:00.41 akifuatiwa na Shuwena Mohamedi wa  Dar es Salaam    01:04.69 huku Veronica Mlonge kutoka  Iringa    01:05.62 na Halima Hamza wa Dar es Salaam      akihitimisha kwa sekunde 01:10.92

Mita 400 Wanaume, Mohamedi Ally Mshambaalishinda akitumia sekunde      50.91 akifuatiwa na Simai Kombo Haji wote Zanzibar sekunde       51.41 wa tatu Twahil Haji Amer  Dar Es Salaam    51.50.

Nafasi ya nne, Jeremiah Baruti akitumia sekunde 51.72, wa tano John Silima   51.88 wote kutoka Dar es Salaam wakati Boaz Benesta kutoka Simiyu alishika nafasi ya sita akitumia sekunde 52.16 na wa saba ni Matondo Magembe pia wa Simiyu        52.38.

Akizungumza mara baada ya mashindano hayo, Mjumbe wa Kamati ya Ufundi RT, Robert Kalyahe, alisema mashindano hayo ni hitimisho la agizo la Rais wa shirikisho, Anthony Mtaka, aliyeitaka na kuiwezesha mikoa kufanya mbio za majaribio kwa ajili ya kusaka wachezaji wa kuunda timu ya Taifa ya Relay kwa mita 100X4 na 400X4.

Alisema RT imeamua kuanza kugeukia mbio za uwanjani, baada ya muda mrefu nguvu kuwa ikiwekezwa kwenye mbio ndefu za barabarani.

Alisema wachezaji wengi wameonyesha ushindani, lakini hawakuweza kufikia viwango vilivyokuwa vimewekwa ambavyo ni sekunde 10.2 hadi 10.6 mita 100 na sekunde 46.5 hadi 47.4 mita 400 wanaume huku kwa wanawake mita 100 ni sekunde 11.4 hadi 12.5 huku mita 400 ni sekunde 52.00 hadi 58.6.

Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais RT-Ufundi, Dk. Hamad Ndee, aliwataka wachezaji kutokata tamaa bali wazidishe kujituma katika mazoezi huku nidhamu ndani na nje ya uwanja ikiwa kipaumbele.

Alisema kwa matokeo yaliyopatikana, angalau kwa wanaume hususa mita 100 waliokimbia chini ya sekunde 11 ambao ni sita wakiandaliwa ipasavyo wanaweza kufikia viwango vilivyokuwa vimewekwa na kuunda timu ya Taifa.

Dk. Ndee, alisema wanaandaa ripoti maalumu kwenda kwa Rais wa RT, ambapo watashauri wanariadha hao sita mita 100 wanaume waliokimbia chini ya sekunde 11, waingie kambini ili kuwanoa waweze kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment

Pages