Mchezo huo wa kuvutia kwa
pande zote mbili, ulifanyika leo Februari 23, 2020 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, na
kuwafanya mabingwa hao mara 27, kutoka uwanjani wakiwa hawaamini.
Sare hiyo ni ya nne
mfululizo kwa Yanga, ambayo imekuwa na matokeo ya ovyo hivi sasa na kujiweka
sehemu mbaya ya kuweza kutwaa taji hilo msimu huu.
Wanajangwani hao walianza
kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, kisha Tanzania Prisons (0-0),
Polisi Tanzania (1-1) na hii ya Coatal Union.
Mwenendo huo mbovu wa
Yanga, unawafanya watani zao, Simba kutanua kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo,
kwa kuwaacha kwa ‘gepu’ kubwa la pointi.
Hivyo basi, matokeo hayo
yanawafanya kuendelea kushika nafasi ya nne, ikiwa na pointi 41, wakicheza
michezo 22, lakini wakiwa na faida ya viporo viwili.
Lakini imeachwa pointi 21
na vinara wa ligi hiyo, Simba ambayo inaongoza msimamo huo wakiwa na pointi 62, baada ya juzi kushinda mechi yake dhidi ya
Biashara United ya Mara.
Mchezo huo ulianza
kwa kasi kwa pande zote mbili, kwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo
safu zao za ushambuliaji zilishindwa kuzitumia.
Katika kipindi cha
kwanza, Yanga ndio iliutawala mchezo, hadi kumiliki mpira kwa asilimia 55
kwa 45 za Coastal Union inayonolewa na Kocha Juma Mgunda.
Kipindi cha pili Coastal
Union ilizinduka zaidi hadi kumaliza dakika 90, wakiwa sawa uwiano wa umiliki
wa mpira wakiwa na 50 kwa 50.
Ni mchezo ambao ulikuwa
bora, lakini jambo ambalo lilikosekana na upachikaji wa mabao tu, kwa vile safu
zote za ushambuliaji zilikosa kuwa makini.
Matokeo mengine ya leo,
Tanzania Prisons waliifumua Lipuli FC, mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Sokoine,
jijini Mbeya, wakati Alliance FC wakilazimishwa sare ya 1-1 na Singida United,
Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.
Golikipa wa Yanga, Metacha Mnata, akimzuia winga wa Coastal Union ya Tanga, Issa Said, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Timu hizo zilitoka suluhu. (Picha na Coastal Union).
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MABINGWA wa kihistoria,
Yanga SC, imezidi kupunguzwa kasi ya kutwaa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), msimu
huu, baada ya jana kulazimisha suluhu dhidi ya wenyeji, Coastal Union ‘Wagosi
wa Kaya’ ya Tanga.
Mchezo huo wa kuvutia kwa
pande zote mbili, ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, na
kuwafanya mabingwa hao mara 27, kutoka uwanjani wakiwa hawaamini.
Sare hiyo ni ya nne
mfululizo kwa Yanga, ambayo imekuwa na matokeo ya ovyo hivi sasa na kujiweka
sehemu mbaya ya kuweza kutwaa taji hilo msimu huu.
Wanajangwani hao walianza
kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, kisha Tanzania Prisons (0-0),
Polisi Tanzania (1-1) na hii ya Coatal Union.
Mwenendo huo mbovu wa
Yanga, unawafanya watani zao, Simba kutanua kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo,
kwa kuwaacha kwa ‘gepu’ kubwa la pointi.
Hivyo basi, matokeo hayo
yanawafanya kuendelea kushika nafasi ya nne, ikiwa na pointi 41, wakicheza
michezo 22, lakini wakiwa na faida ya viporo viwili.
Lakini imeachwa pointi 21
na vinara wa ligi hiyo, Simba ambayo inaongoza msimamo huo wakiwa na pointi 62, baada ya juzi kushinda mechi yake dhidi ya
Biashara United ya Mara.
Mchezo huo ulianza
kwa kasi kwa pande zote mbili, kwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo
safu zao za ushambuliaji zilishindwa kuzitumia.
Katika kipindi cha
kwanza, Yanga ndio iliutawala mchezo, hadi kumiliki mpira kwa asilimia 55
kwa 45 za Coastal Union inayonolewa na Kocha Juma Mgunda.
Kipindi cha pili Coastal
Union ilizinduka zaidi hadi kumaliza dakika 90, wakiwa sawa uwiano wa umiliki
wa mpira wakiwa na 50 kwa 50.
Ni mchezo ambao ulikuwa
bora, lakini jambo ambalo lilikosekana na upachikaji wa mabao tu, kwa vile safu
zote za ushambuliaji zilikosa kuwa makini.
Matokeo mengine ya jana,
Tanzania Prisons waliifumua Lipuli FC, mabao 2-0, kwenye Uwanja wa Sokoine,
jijini Mbeya, wakati Alliance FC wakilazimishwa sare ya 1-1 na Singida United,
Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment